Wilaya ya Meatu
Wilaya ya Meatu ni wilaya mojawapo kati ya wilaya sita za Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39400 [1].
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 299,619 [2]. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 366,941 [3].
Makao makuu ya wilaya yapo Mwanhunzi.
Eneo lake ni kilomita za mraba 8,835.
Mipaka
[hariri | hariri chanzo]Meatu imepakana na Wilaya ya Bariadi upande wa kaskazini, Wilaya za Karatu, Ngorongoro na Mbulu upande wa mashariki, Mkoa wa Singida na Maswa upande wa magharibi na Shinyanga upande wa kusini.
Maeneo ya kuhifadhiwa
[hariri | hariri chanzo]Karibu nusu ya wilaya ni maeneo yaliyohifadhiwa ambayo ni
- Hifadhi ya wanyama ya Maswa (2,094 km2) na
- Makao Open Area (kata ya Mwangundo, 1,330 km2)
- sehemu za Hifadhi ya Serengeti (694 km2 ndani ya wilaya)
- sehemu za Hifadhi ya Ngorongoro (135 km2 ndani ya wilaya)
Maeneo mengine ya km2 4,582 ni ardhi ya kilimo na ufugaji.[4]
Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Eneo la Meatu ni nusu yabisi yaani haipokei mvua nyingi. Kiwango cha mvua kinapungua kutoka kaskazini kuelekea upande wa kusini ambako ni milimita 400 pekee zinazonyesha kwa mwaka ilhali sehemu za kaskazini zinapokea milimita 900. [5] Kiwango cha mvua huweza kuwa tofauti kila mwaka ambayo ni tatizo kwa ajili ya wakulima.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi kwa jumla ni wa kilimo na ufugaji. Mazao ya chakula ni hasa mahindi na mtama lakini kilimo cha mahindi huwa na matatizo ya mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya kiwango cha mvua. Kwa hiyo kila baada ya miaka mitano kuna uhaba wa chakula. Wanawake hulima mahali pengi viazi vitamu karibu na mito ya muda mahali ambako ipo.
Udongo hasa upande wa kusini una kiwango kikubwa mno cha magadi na hivyo hufai kwa kilimo cha muhogo ambalo ni zao linalovumulia ukame.
Ufugaji ni muhimu katika wilaya na wastani ya ng'ombe ni 12-13 kila kaya lakini kwa tofauti kati ya ng'ombe 0 na 2,00 kwa kaya.
Zao la biahara muhimu zaidi ni pamba. Watu wameanza kujenga vinu vya kuchambulia pamba kwa hiyo soko la pamba limeboreshwa hata kama mwendo huu unaweza kuleta matatizo ya chakula. Meatu ni eneo lenye pamba nyingi katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga.
Utalii ni tawi la uchumi lililoanza kuchipuka kutokana na nafasi ya kuwinda.
Uchimbaji wa vito umeanza hapa na pale kwa kutumia mbinu za kienyeji.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Sensa ya 2012, Simiyu Region - Meatu District Council
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Site Report for Nzanza Village Meatu District, uk.5
- ↑ Site Report for Nzanza Village Meatu District, uk.5
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Meatu District Profile, katika: Site Report for Nzanza Village Meatu District Ilihifadhiwa 4 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- Village Reports for Mbushi, Iramba Ndogo, Sapa, and Makao in Meatu District
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Meatu - Mkoa wa Simiyu - Tanzania | ||
---|---|---|
Bukundi | Imalaseko | Isengwa | Itinje | Kabondo | Kimali | Kisesa | Lingeka | Lubiga | Mbugayabanghya | Mbushi | Mwabuma | Mwabusalu | Mwabuzo | Mwakisandu | Mwamalole | Mwamanimba | Mwamanongu | Mwamishali | Mwandoya | Mwangudo | Mwanhuzi | Mwanjolo | Mwanyahina | Mwasengela | Ng'hoboko | Nkoma | Sakasaka | Tindabuligi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |