Wilaya ya Chemba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Wilaya ya Chemba
Mahali paWilaya ya Chemba
Mahali paWilaya ya Chemba
Mahali pa Chemba mkoani Dodoma
Majiranukta: 05°14′34″S 35°53′24″E / 5.24278°S 35.89000°E / -5.24278; 35.89000Coordinates: 05°14′34″S 35°53′24″E / 5.24278°S 35.89000°E / -5.24278; 35.89000
Nchi Tanzania
Mikoa Mkoa wa Dodoma
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 339,333

Chemba ni jina la wilaya mpya katika mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 41800[1], ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega wilaya ya Kondoa[2].

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Chemba inapakana na wilaya ya Kondoa upande wa kaskazini, mkoa wa Manyara upande wa mashariki, wilaya ya Chamwino na wilaya ya Bahi upande wa kusini, na mkoa wa Singida upande wa magharibi.

Makao makuu ya wilaya yako Chemba.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya sensa ya mwaka 2012, wilaya ya Chemba ilikuwa na wakazi 235,711.[3] Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 339,333 [4].

Wakazi wengi wa Chemba ni wakulima na wafugaji na mazao yao ni kama vile mahindi, ulezi, alizeti, uwele, udo. Wanyama wanaofugwa ni kama vile ng'ombe, mbuzi, punda na kondoo.

Chemba ni miongoni mwa sehemu ambazo zipo nyuma sana kielimu, pia eneo hili lina shida kubwa ya maji katika vijiji vyake vyote.

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Barabara T5 kutoka Dodoma hadi Babati inapitia wilaya hii.[5]

Ugatuzi[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa Wilaya ya Chemba inajumuisha tarafa za Goima, Mondo, Kwamtoro na Farkwa pamoja na kata zake 26.[3]

Kata[hariri | hariri chanzo]


Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
  2. New constituencies up for grabs as CUF cries foul. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-20. Iliwekwa mnamo 21 July 2016.
  3. 3.0 3.1 Census 2012. Iliwekwa mnamo 21 July 2016.
  4. https://www.nbs.go.tz
  5. Dodoma Roads Network. Jalada kutoka ya awali juu ya 24 June 2016. Iliwekwa mnamo 17 June 2016.
Kata za Wilaya ya Chemba - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Babayu | Chandama | Chemba | Churuku | Dalai | Farkwa | Goima | Gwandi | Jangalo | Kidoka | Kimaha | Kinyamsindo | Kwamtoro | Lahoda | Lalta | Makorongo | Mondo | Mpendo | Mrijo | Msaada | Ovada | Paranga | Sanzawa | Songolo | Soya | Tumbakose


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Chemba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.