Sanzawa
Sanzawa ni jina la kata ya Wilaya ya Chemba katika Mkoa wa Dodoma , Tanzania yenye postikodi namba 41811[1] . Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10613 [2] waishio humo.
Sanzawa ipo katika tarafa ya Kwamtoro. Ina jumla ya vitongoji vinane. Wakazi wake ni wasandawe, wagogo na wabarabaig. Wakazi wa Sanzawa wanajishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, uwele, mtama, udo, mihogo n.k. Mazao ya biashara ni alizeti, ufuta na karanga.
Wakazi wa Sanzawa pia ni wafugaji wa mifugo mbalimbali. Hali ya hewa ya Sanzawa ni nusu jangwa hivyo hukabiliwa na ukame na hali ya ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu. Hivyo kwa wafugaji hutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili mifugo yao.
Sanzawa pia ni makao makuu ya kata. Hivyo ina shule ya sekondari ya kata.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
- ↑ Sensa ya 2012, Dodoma - Chemba DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
![]() |
Kata za Wilaya ya Chemba - Mkoa wa Dodoma - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Babayu | Chandama | Chemba | Churuku | Dalai | Farkwa | Goima | Gwandi | Jangalo | Kimaha | Kwamtoro | Kidoka | Kinyamsindo | Lahoda | Lalta | Makorongo | Mondo | Mpendo | Mrijo | Msaada | Ovada | Paranga | Sanzawa | Songoro | Soya | Tumbakose |