Job Yustino Ndugai

Job Yustino Ndugai (21 Januari 1960 – 6 Agosti 2025) alikuwa mbunge wa jimbo la Kongwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[1] Alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Maisha na kazi
Job Ndugai alihudumu kama mbunge wa jimbo la Kongwa kuanzia mwaka 2000 hadi kifo chake mwaka 2025. Tangu tarehe 17 Novemba 2015 hadi 6 Januari 2022 alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Kabla ya hapo, alikuwa Naibu Spika wa Bunge hilo kuanzia mwaka 2010.
Mnamo Januari 2022, alijiuzulu wadhifa wake wa uspika baada ya kutokea mvutano wa kisiasa na rais Samia Suluhu Hassan.[2]
Elimu
Job Ndugai alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya Sekondari ya Kibaha na baadaye kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambako alisomea sayansi ya wanyama. Pia alisomea masuala ya bunge katika vyuo vya kimataifa ikiwa ni pamoja na India na Ujerumani.
Tazama pia
Marejeo
- ↑ "Mengi kuhusu Job Yustino Ndugai". 13 Julai 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-27. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2011.
- ↑ BREAKING: Tanzania's Speaker of Parliament Job Ndugai has resigned, The Citizen, tar. 6 Januari 2022
| Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Job Yustino Ndugai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |