Wilaya ya Kaliua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Kaliua katika Mkoa wa Tabora

Wilaya ya Kaliua ni moja ya wilaya katika Mkoa wa Tabora, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kutoka maeneo ya wilaya ya Urambo[1]. Postikodi zake huanza kwa namba 457.

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Maeneo ya wilaya hiyo ni kilomita za mraba 14,050. Makao makuu yako kwenye mji wa Kaliua takriban km 125 kutoka Tabora. Wilaya inapakana na Urambo na Wilaya ya Uyui upande wa mashariki, Wilaya ya Mpanda (Mkoa wa Katavi) upande wa kusini, Uvinza na Kibondo (Kigoma) upande wa magharibi. Upande wa kaskazini Wilaya inapakana na Ushetu (Shinyanga) na Bukombe (Geita) upande wa kaskazini-magharibi.

Tabianchi[hariri | hariri chanzo]

Tabianchi huonyesha jotoridi baina 16-33, kiwango cha mvua ni ya mm 900-1300 kwa mwaka.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kilimo cha Kaliua ni mazao kama mahindi, maharagwe, mhoji na viazi vitamu pamoja na tumbaku, karanga, pamba na alizeti halafu asali na mifugo. Sekta ya kilimo huajiri asilimia 80 ya idadi ya watu wa Kaliua.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. History, tovuti rasmi ya Wilaya

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1], tovuti rasmi ya Wilaya
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Kaliua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Kata za Wilaya ya Kaliua - Mkoa wa Tabora - Tanzania

Ichemba | Igagala | Igombemkulu | Igwisi | Ilege | Kaliua | Kamsekwa | Kanoge | Kashishi | Kazaroho | Kona Nne | Makingi | Milambo | Mkindo | Mwongozo | Nhwande | Sasu | Seleli | Silambo | Ufukutwa | Ugunga | Ukumbi Siganga | Usenye | Ushokola | Usimba | Usinge | Uyowa | Zugimlole