Kaliua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kaliua
Kaliua is located in Tanzania
Kaliua
Kaliua

Mahali pa Kaliua katika Tanzania

Majiranukta: 5°3′32″S 31°47′36″E / 5.05889°S 31.79333°E / -5.05889; 31.79333
Nchi Tanzania
Mkoa Tabora
Wilaya Urambo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 17,073

Kaliua ni jina la makao makuu ya Wilaya ya Kaliua katika Mkoa wa Tabora, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,073 waishio humo.[1]

Wilaya hiyo mpya ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012. Kaliua ipo njia panda ya reli iendayo Kigoma kwa upande wa magharibi na Mpanda kwa upande wa kusini. Kaskazini imepakana na wilaya ya Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.

Wilaya ya Kaliua ina uwanja wa ndege mdogo kwa shuguli ndogondogo za anga. Ina huduma za simu za mkononi, posta, shule za sekondary ikiwa ni pamoja na Kaliua high school. Kwa ujumla ni mji unaokuwa kwa kasi sana ktk ukanda huo wa magharibi.

Kwenye mwaka 2013 mbunge wa wilaya hiyo alikuwa mh.profesa Juma Athumani Kapuya. Aliwahi kuwa waziri wa elimu, kazi na maendeleo ya vijana, wizara ya ulinzi n.k.

Mazao yanayolimwa Kaliua ni tumbaku, karanga, mahindi, alizeti, ufuta. Ufugaji ni muhimu. Asali ni moja ya zao linalovunwa saana kaliua, pia uvuvi hufanyika katika maeneo oevu ya usinge, swampu nk.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kaliua - Mkoa wa Tabora - Tanzania

Ichemba | Igagala | Igombemkulu | Igwisi | Ilege | Kaliua | Kamsekwa | Kanoge | Kashishi | Kazaroho | Kona Nne | Makingi | Milambo | Mkindo | Mwongozo | Nhwande | Sasu | Seleli | Silambo | Ufukutwa | Ugunga | Ukumbi Siganga | Usenye | Ushokola | Usimba | Usinge | Uyowa | Zugimlole


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kaliua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.