Gombe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sokwe wa hifadhi ya Gombe.
Sokwe anayekula.

Gombe ni hifadhi ya taifa katika nchi ya Tanzania. Ni hifadhi ndogo kuliko zote nchini ikiwa na kilometa za mraba 52 tu, lakini ina umaarufu mkubwa unaotokana na kivutio chake kikubwa ambacho ni sokwe.

Iko umbali wa kilometa 16 kaskazini kwa mji wa Kigoma

Hifadhi hii ni ukanda mwembamba wa msitu wa mlimani unaokatizwa na miteremko mikali inayoingia katika mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Gombe ni miongoni mwa makazi machache yaliyosalia ya sokwe duniani. Hifadhi hii ilipata hasa umaarufu baada ya mtafiti wa tabia ya sokwe duniani, Jane Goodall kufanya utafiti juu ya maisha na tabia za sokwe wa Gombe kwa miaka 40 na kuandika vitabu kadhaa kuhusu viumbe hao.

Wanyama wengine wanaopatikana katika hifadhi hii ni pamoja na kima wenye mikia myekundu na kima wa bluu.

Wanyama wa jamii ya paka, kama chui na simba hawapo katika hifadhi hii na hivyo kuifanya kuwa salama kwa safari za miguu.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni wakati wa kiangazi, Julai-Oktoba kwa sababu sokwe hawapendi kutembea nyakati za mvua.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: