Mlima Meru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mlima Meru, 2012
Mlima Meru kutoka juu

Mlima Meru ni mlima wa volkeno na una urefu wa mita 4565 (futi 15064) kutoka usawa wa bahari. Mlima huu ni wa tano kwa urefu katika bara la Afrika.

Mlima Meru unapatikana ndani ya Hifadhi ya Arusha ambayo ilianzishwa mwaka 1960 ambapo wanyama pori kuzunguka Maziwa ya Momella na Volcano ya Ngurudoto (Ngurudoto crater) walihifadhiwa na kulinwa katika eneo hili.

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 137 na ipo umbali wa kilometa 35 kutoka katika mji wa kitalii wa Arusha na Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.

Kilele cha Mlima Meru

Vivutio katika hifadhi hii vinajumuisha volkeno, maziwa, misitu na wanyama pori kama twiga, tembo, pundamilia, nyati na wengine wengi. Pia kuna ndege wa aina nyingi wakiwemo flamingo, pia misitu katika mlima Meru ni makazi ya nyani.

Kupanda Mlima Meru inachukua siku tatu hadi nne na wakati mzuri wa kupanda mlima ni kuanzia mwezi Juni hadi Februari ambapo mvua zinaweza kunyesha katika mwezi wa Novemba. Na wakati mzuri wa kuona Kilimanjaro kutokea Meru ni mwezi kati ya Desemba na Februari.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya Utalii na maliasili za Tanzania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]