Hifadhi ya Arusha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Chui katika mawindo

Hifadhi ya Arusha inapatikana katika mji wa Arusha nchini Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 542, iko umbali wa kilometa 32 kutoka katika mji wa kitalii wa Arusha.

Maeneo makubwa na muhimu ya hifadhi[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama jamii ya tumbili wajulikanao kama mbega weusi na weupe. Wanyama wengine wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi hii ni pamoja na twiga, pundamilia, nyati na digidigi. Aidha unaweza kuwaona chui wakibarizi katika vivuli vya matawi ya miti inayokingwa na maanguko ya maji huku makundi kadhaa ya batamaji yakitafuta wadudu katika maziwa ya Momella.

Zaidi ya aina 400 za ndege wamethibitika kupatikana ndani ya hifadhi hii.

Mambo yanayoweza kufanyika ndani ya hifadhi hii[hariri | hariri chanzo]

Safari za miguu na kupanda mlima Meru ni moja ya burudani muhimu katika hifadhi hii, na mpandaji anahitaji siku 3-4 za kupanda mlima.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kati ya mwezi Juni na Februari ingawa mvua inaweza kunyesha mwezi novemba.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]