Digidigi
Jump to navigation
Jump to search
Digidigi | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Digidigi wa Kirk
(Madoqua kirkii) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Digidigi ni wanyamapori wadogo wa jenasi Madoqua katika familia Bovidae. Wanyama hawa ni miongoni mwa wanyama wadogo kabisa wa Bovidae (kimo sm 30–40 begani, urefu sm 50–70 na uzito kg 3–6). Wanatokea savana kavu za Afrika kusini kwa Sahara. Jike ni mkubwa kidogo kuliko dume lakini dume ana pembe fupi na nyembamba. Wana ushungi kwa utosi unaoficha pengine pembe za dume. Rangi yao ni ya mchanga lakini mgongo una rangi ya majivu. Digidigi hula majani, matunda na beri. Wanapata maji ya kutosha kutoka chakula chao, kwa hivyo hawana haja ya kunywa.
Spishi[hariri | hariri chanzo]
- Madoqua guentheri, Digidigi wa Günther (Günther's Dik-dik)
- Madoqua kirkii, Digidigi wa Kirk (Kirk's Dik-dik)
- Madoqua piacentinii, Digidigi Fedha (Silver Dik-dik)
- Madoqua saltiana, Digidigi wa Salt (Salt's Dik-dik)
Picha[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Digidigi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.