Kulungu Mwekundu wa Atlas
Kulungu mwekundu wa Atlas | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kulungu mwekundu wa Atlas (Cervus corsicanus)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Kulungu mwekundu wa Atlas ni mnyama mkubwa wa jenasi Cervus katika familia Cervidae anayetokea Afrika ya kaskazini magharibi na visiwa vya Korsika na Sardinia. Zamani alifikiriwa kuwa nususpishi ya kulungu mwekundu wa Ulaya (Cervus elaphus barbarus), lakini wanyama wa Afrika wana mnasaba karibu na wale wa Korsika na Sardinia. Uchunguzi wa ADN unapendekeza kwamba wanyama hawa ni spishi tofauti.
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Kulungu huyu ni mdogo kuliko yule wa Ulaya. Rangi ya mwili ni kahawia na kuna madoa meupe kwenye mbavu na mgongo. Hakuna tawi la pili juu ya pembe zake.
Msambao
[hariri | hariri chanzo]Spishi hii ni kulungu wa pekee wa Cervidae ambaye anatokea Afrika, katika misitu ya Aljeria, Maroko na Tunisia. Kuhusu nadharia moja watu wa zamani sana wamewasilisha spishi hii kwenye visiwa vya Korsika na Sardinia. Huko Maroko kulungu walimalizwa kwa uwindaji, lakini wanyama wengine waliwasilishwa kutoka Tunisia wakati wa miaka 1990[1]
Maadui
[hariri | hariri chanzo]Maadui wa kulungu mwekundu wa Atlas ni au walikuwa simba wa Barbari, dubu wa Atlas na chui wa Barbari, lakini wanyama hawa wamekwisha sasa au wamekuwa nadra.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kitomeo cha Fish & Wildlife Service ya MMA kuhusu kulungu mwekundu wa Atlas
- Maelezo Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. (Kihispania)
- Kujumuisha kwa Cervus elaphus barbarus katika kiambatisho I cha CITES Ilihifadhiwa 15 Juni 2010 kwenye Wayback Machine. (pamoja na maelezo ya spishi hii)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Le programme d'espèces d'UICN et la Commission UICN de la sauvegarde des espèces et TRAFFIC. "Résumés des Analyses UICN/TRAFFIC des propositions d'amendement aux Annexes de la CITES pour la Quatorzième session de la Conférence des Parties", Retrieved on 2008-12-28.
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.