Nenda kwa yaliyomo

Swala pala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Aepyceros)
Swala pala
Swala pala wa kawaida (Aepyceros m. melampus)
Swala pala wa kawaida
(Aepyceros m. melampus)
Swala pala uso-mweusi (Aepyceros m. petersi)
Swala pala uso-mweusi
(Aepyceros m. petersi)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Aepycerotinae (Swala pala)
J. E. Gray, 1872
Jenasi: Aepyceros
Sundevall, 1847
Spishi: A. melampus
Lichtenstein, 1812
Ngazi za chini

Nususpishi 2:

Swala pala au swalapala (Aepyceros melampus kutoka Kigiriki αιπος, aipos "juu" κερος, ceros "pembe" + melas "nyeusi" pous "mguu") ni swala ambaye si mkubwa sana kutoka Afrika. Jina Impala ambalo ni jina la swala pala kwa Kiingereza linatoka kutoka lugha ya Kizulu na linamaanisha "Swara". Wao hupatikana katika savana misitu nene nchini Kenya, Tanzania, Eswatini, Msumbiji, Namibia ya kaskazini, Botswana, Zambia, Zimbabwe, kusini mwa Angola, kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini na Uganda. Swala pala wa kawaida wanaweza kupatikana katika idadi ya hadi 1,600,000 barani Afrika.[1]

Uainishaji

[hariri | hariri chanzo]

Hapo awali, wanataksonomia waliwaweka swala pala katika jamii sawa na swala, ndogoro na kongoni. Hata hivyo ilikuja kugunduliwa kwamba swala pala ni tofauti sana kutoka jamii hizi zote za swala ndiposa swala pala ikawekwa katika jamii yake yenyewe, Aepycerotini, mtawalia. Jamii hii kwa sasa imepandishwa cheo kuwa nusufamilia kamili, Aepycerotinae.

Kwa kawaida nususpishi mbili hutofautishwa, ambazo huegemezwa na uchambuzi wa mitochondrial DNA.

Mwonekano

[hariri | hariri chanzo]
Swala pala dume kutoka Kruger National Park, Afrika ya Kusini.

Swala pala wana urefu wa kati ya sentimita 73 na 92. Wastani wa uzito wa swala pala wa kiume ni takriban kilo 46 hadi 76 huku swala pala wa kike wakiwa na uzito wa takriban kilo 37 hadi 50. Rangi yao kwa kawaida ni nyekundu na kahawia (ndiposa wakapewa jina la Kiafrikana la "Rooibok" ), wana ubavu mwepesi na tumbo nyeupe alama "M" katika ngozi zao. Swala pala wa kiume, ambao wana jina sawa kama wa kondoo waume, wana pembe zinazofanana kama aina fulani ya chombo cha muziki kinachojulikana kama 'lyre' kwa lugha ya kimombo, na zinaweza kufikia urefu wa sentimita 90. Swala pala wa kike, ambao wana jina sawa na kondoo wa kike, hawana pembe.

Swala pala weusi

[hariri | hariri chanzo]

Swala pala weusi, hupatikana katika maeneo machache sana barani Afrika, na aina ya swala pala hawa ni nadra sana na wana mwili ambao ni mweusi. Hifadhi ya wanyama ya kibinafsi ya Botlierskop Binafsi nchini Afrika Kusini ina zaidi ya swala pala weusi 150 na hata zaidi ya swala pala wekundu. Wanyama hawa wanaweza kufomu makundi makubwa ya zaidi ya swala pala 100, lakini kwa kawaida idadi ya mkusanyiko wao huwa 20. Kidude cha ukoo kinachopatikana katika swala pala huwapa rangi yao.

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Swala pala ni miongoni mwa spishi ambao wametamalaki katika aina nyingi za savana. Wanaweza kukabiliana na mazingira tofauti kwa kuwa walaji wa nyasi katika baadhi ya maeneo. Wao hula majani na nyasi wakati rangi ya majani na nyasi ni kijani na ambao unakuwa.

Vikundi vya swala pala hutumia maeneo maalumu kwa matumizi yao. Swala pala huwa hodari wakati wote wa usiku na mchana na wanategemea maji. Mifugo ni huashiria kwa kawaida kuwa kuna maji karibu. Swala pala wanaweza kustawi katika maeneo ambayo walaji nyasi pekee hawezi kuishi.

Swala pala mke kutoka kwa Kruger National Park, Afrika ya Kusini.

Swala pala hurukaruka huku na huko ili kuwavuruga wanyama ambao wanaweza kuwala. Wao wanaweza kuruka kwa umbali wa zaidi ya mita 10 (futi 33) na urefu wa mita 3 (futi 9). Chui, duma, simba na mbwa mwitu ndio wanyama ambao huwawinda Swala pala. Swala pala wanaweza kufikia kasi ambao wastani wake ni maili 50 hadi 55 kwa saa moja (kilomita 80 hadi 90 kwa saa moja)[2] ili kuwaepuka wanyama ambo wanaweza kuwala.

Muundo wa kijamii na uzazi

[hariri | hariri chanzo]

Swala pala wa kike na swala pala wale wachanga kufomu vikundi vya swala pala mia moja au mia mbili. Wakati wa chakula upo kwa wingi, swala pala wazima wa kiume wataimarisha wilaya na kuwazunguka swala pala wa kike na kuwafukuza swala pala wa kike ambao si wa jamii ya kundi hilo, pamoja na wanyama wengine ambao wanaweza kuwala. Pia wao huwafukuza swala pala wa kiume wengine ambao wamebalehe. Swala pala wa kiume hujaribu kuzuia swala pala yeyote wa kike anayejaribu kuondoka katika wilaya ambao walikuwa wameutenga. Katika misimu wa ukavu, wilaya hizi hutelekezwa na kuachwa kwani vikundi hivi vya swala pala husafiri mbali ili kutafuta chakula. Vikundi vikubwa vya swala pala huanzishwa na hujumuisha swala pala wa kike na wa kiume.

Swala pala vijana wa kiume ambao wamefanywa kuacha vikundi vyao vya awali hufomu kundi yao ya karibu takriban swala pala thelathini binafsi. Swala pala wa kiume ambao wanaweza kutawala na kutamalaki vikundi vyao huwa wagombeaji kwa ajili ya kuchukua udhibiti wa wilaya zao.

Swala pala kurukaruka huku nchini Kenya.

Msimu wa kuzaana wa swala pala, ambao pia hujulikana kama rutting kwa lugha ya Kiingereza, huanza wakati unaelekea mwisho wa msimu wa mvua mwezi wa Mei. Mambo haya yote kwa kawaida hudumu kwa muda wa takriban wiki tatu. Huku swala pala wachanga wakizaliwa baada ya miezi saba, mama yao ana uwezo wa kuchelewa kujifungua kwa nyongeza ya mwezi moja kama hali ni mbaya. Wakati wa kujifungua swala pala wa kike hujitenga mwenyewe kutoka katika kundi ya swala pala wengine licha ya jitihada mbalimbali ya swala pala wa kiume kumzuia kuondoka katika wilaya yao. Swala pala wa kike ambaye amekuwa mama kumweka mwanawe aliyezaliwa katika doa kwa siku chache au hata kumwacha mwanawe mafichoni kwa siku, wiki kadhaa au zaidi kabla ya kurudi kwa kundi la swala pala wenzake. Wanawe wachanga watajiunga na kikundi cha swala pala wengine na watakwenda kwa mamao tu wakati kuna shida au wakati wana njaa na wanahitaji kula. Swala pala wachanga hunyonya matiti ya mamao kwa muda wa kati ya miezi 4 hadi 6. Swala pala wa kike ambao hukomaa wanalazimika kujiondoa katika kikundi hicho na kujiunga na kundi mpya ya swala pala ya wanaume pekee.

Hifadhi ya picha

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.iucnredlist.org/apps/redlist/details/550/0/full
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-20. Iliwekwa mnamo 2011-01-19.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.