Elki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elki
Elki (Alces alces)
Elki
(Alces alces)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Artiodactyla (Mamalia wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili)
Nusuoda: Ruminantia
Familia: Cervidae (Wanyama walio na mnasaba na kulungu)
Nusufamilia: Capreolinae (Wanyama wanaofanana na kulungu wa Dunia Mpya)
Jenasi: Alces
J.E. Gray, 1821
Spishi: A. alces
(Linnaeus, 1758)
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Elki (kutoka Kiing.: elk, Kisayansi: Alces alces) ni spishi kubwa katika familia Cervidae. Elki wanajulikana kwa kichwa chake kikubwa na pembe-tawi zake zinazogawanyika kama vidole vya kiganja; spishi nyingine za familia hii huwa na pembe-tawi zinazogawanyika katika matawi. Kwa kawaida elki huishi misituni mwa kaskazini na misitu yenye miti ya kupukutika majani yake ya Nusudunia ya kaskazini katika hali za nchi za wastani hadi maeneo ya chini ya Aktiki. Kutokana na uwindaji, elki wana makazi madogo zaidi. Sasa elki wengi wanapatikana Kanada, Alaska, Skandinavia na Urusi. Wao hula mimea ya ardhini na majini. Wanyama ambao huwinda elki ni mbwa-mwitu, dubu na binadamu. Tofauti na spishi zingine za kulungu, elki ni wanyama pweke na huwa hawaishi na kundi la elki wengine. Ingawa elki kwa kawaida hutembea polepole, wakasirishwapo elki waweza kuwa mkali na kusonga haraka. Wakati wa demani iliye majira yao ya kupandana, madume wa spishi hupigana na madume wengine na kumshindania jike.

Etimolojia na jina[hariri | hariri chanzo]

Jina elki limekopwa kutoka Kiingereza. Katika Uingereza mnyama huyu huitwa elk, lakini katika Amerika huitwa moose na elk huko ni jina la wapiti. Jina la kisanayansi "alcus" siyo Kilatini lakini limekopwa kutoka Kiswidi älg.

Elki dume aliyekua hurejelewa kama fahali, na elki jike ni dachia, na mtoto wa elki ni ndama.

Makazi na eneo[hariri | hariri chanzo]

Amerika Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Katika Amerika Kaskazini, elki huishi Kanada (mbali na Aktiki), Alaska, Uingereza Mpya, Milima yenye Miamba, Minesota, Peninsula ya Juu ya Michigan na Kijisiwa cha Kifalme cha Ziwa Kubwa. Katika eneo hili kubwa, kuna nususpishi zingi. Katika magharibi ya bara ya Amerika Kaskazini, idadi za elki zinafikia kaskazini mwa Kanada (Kolumbia ya Kibritania na Alberta) na spishi wengine wamepatikana milimani mwa Utah na Kolorado.

Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Katika Ulaya, elki wanapatikana katika Norwe, Uswidi, Ufini, Urusi, Polandi na nchi za Kibalti, na elki wachache katika Ucheki, Belarusi na Ukraini.