Alpaka
Alpaka | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Alpaka asiyenyoleka akila
(Vicugna pacos) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Msambao wa alpaka
|
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alpaka ni mnyama wa kufugwa wa spishi Vicugna pacos katika familia Camelidae, anayeishi Amerika Kusini. Alpaka anafanana na lama mdogo, lakini ameainishwa katika jenasi tofauti. Kuna nususpishi mbili za alpaka; alpaka suri na alpaka huacaya.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Kwa kawaida, alpaka mzima ana kimo cha sm 81–99 mabegani, na uzito wa kilo 48–84.
Alpaka hutunzwa kwa makundi na hulishwa katika nyanda za juu za milima ya Andes katika upande wa kusini wa Peru, kaskazini ya Bolivia, Ekuador, na kaskazini ya Chile, ambako wanaishi mita 3,500–5,000 juu ya usawa wa bahari, mwaka wote.[1] Alpaka ni wadogo kiasi kuliko lama, na tofauti na lama, hawakufugwa kuwa wanyama wa mizigo, badala yake walifugwa mahususi kwa ajili ya manyoya yao. Manyoya ya alpaka hutumiwa kutengeneza vitu vifumwavyo, mithili ya sufu. Vitu hivyo ni pamoja na mablanketi, sweta, kofia, glavu na nguo nyingine katika Amerika Kusini, na sweta, soksi, koti na matandiko katika sehemu nyingine duniani. Fumwele za manyoya yao zinapatikana katika zaidi ya rangi 52, kama zinavyoainishwa Peru.
Katika biashara ya vitambaa, maana ya msingi ya "alpaca" ni nywele za alpaka wa Peru lakini, kwa upana zaidi, "alpaca" inamaanisha mtindo wa vitambaa vilivyotengenezwa awali kutoka nywele za alpaka, ambavyo sasa vinatengenezwa mara nyingi kwa fumwele zinazofanana na nywele za alpaka, kama sufu za ubora sana.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Harvesting of textile animal fibres". UN Food and Agriculture Organization.
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.