Nyamera (jenasi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Beatragus)
Nyamera
Nyamera wa kawaida (Damaliscus korrigum jimela)
Nyamera wa kawaida
(Damaliscus korrigum jimela)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Alcelaphinae (Wanyama wanaofanana na kongoni)
Brooke, 1876
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 5, nususpishi 6:

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyamera ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Beatragus na Damaliscus katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi D. korrigum topi, lakini siku hizi spishi na nususpishi zote huitwa nyamera mara nyingi. Majina mengine ni hirola, jimela, sasabi na tiang. Wanatokea savana za Afrika tu. Rangi yao ni ya mchanga inayoelekea nyekundu au kijivu mara nyingi. Wana mabaka meusi mwilini, miguuni na kichwani, isipokuwa hirola, na nyamera baka-nyeupe ana baka nyeupe kwa pua na paji. Kichwa chao ni kirefu kama kile cha kongoni lakini pembe zao hazina umbo wa zeze. Wanyama hawa hula manyasi.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyamera (jenasi) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.