Nenda kwa yaliyomo

Kulungu Aktiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kulungu Aktiki
Kulungu Aktiki (Rangiferus tarandus)
Kulungu Aktiki (Rangiferus tarandus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Artiodactyla (Mamalia wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili)
Familia: Cervidae (Wanyama walio na mnasaba na kulungu)
Nusufamilia: Capreolinae (Wanyama wanaofanana na kulungu wa Dunia Mpya)
Jenasi: Rangifer
C.H. Smithh, 1827
Spishi: R. tarandus
(Linnaeus, 1758)
Ngazi za chini

Nususpishi 17:

Msambao wa kulungu aktiki
Msambao wa kulungu aktiki

Kulungu aktiki (Kilat.: Rangifer tarandus), anayejulikana kama karibu katika Amerika ya Kaskazini, ni spishi ya kulungu anayeishi ukanda wa Aktiki na maeneo ya chini ya Aktiki. Kuna nususpishi 17, lakini 2 zimekwisha sasa.

Aina za kulungu aktiki hutofautiana kwa rangi na ukubwa. Kwa kawaida jinsia mbili huzaa pembeshada, ingawa pembeshada za madume ni kubwa kuliko zile za jike. Hata hivyo, kuna idadi chache za kulungu aktiki ambazo jike wao hawana pembeshada kabisa.

Uwindaji wa kulungu aktiki wa mwitu na uchungaji wa kulungu aktiki wafugwao kwa nusu (ili kupata nyama, ngozi, pembeshada na maziwa) ni muhimu kwa watu wa Aktiki na maeneo ya chini ya Aktiki kama Waeskimo. Hata nje ya makazi yake, kulungu aktiki anajulikana sana kutokana na Baba Krismasi ambaye sleji yake inayokokotwa na kulungu aktiki wanaoruka angani. Katika Ulapi, kulungu aktiki kokota pulka (aina ya sleji ya Kilapi).

Kulungu aktiki wanaokokota sleji


Makazi[hariri | hariri chanzo]

Kulungu aktiki huishi kaskazini mwa Holaktiki wakipatikana tundra na taiga (msitu wa kaskazini). Kwa asili, kulungu aktiki walipatikana Skandinavia, Ulaya wa Mashariki, Grinlandi, Urusi, Mongolia na Uchina wa kaskazini. Katika Amerika Kaskazini, walipatikana Kanada, Alaska (Marekani), na pia kutoka kaskazini mwa Washington hadi Maine. Karne ya 19, bado walipatikana Idaho. Hata nyakati za kihistoria, waliishi Ayalandi. Wakati wa mwisho wa enzi ya Pleistosini, kulungu aktiki walipatikana hadi umbali wa Nevada na Tenesii katika Amerika Kaskazini na Uhispania katika Ulaya. Sasa kulungu aktiki wa mwitu wametoweka maeneo mengi kati ya eneo hili la kihistoria, hasa sehemu za kusini ambapo walitoweka kabisa. Idadi kubwa ya kulungu aktiki wa mwitu bado hupatikana Unorwe, Ufini, Siberia, Grinlandi, Alaska na Kanada.

Mofolojia[hariri | hariri chanzo]

Ukubwa[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida majike hupima 162-205cm kwa urefu na 80-120kg kwa uzito. Madume (au “fahali”) kwa kawaida wakubwa zaidi wakipima 180-214 kwa urefu na kwa kawaida 159-192kg kwa uzito ingawa madume walio wakubwa sana waweza kuwa na uzani wa 318 kg.

Manyoya[hariri | hariri chanzo]

Rangi ya manyoya inatofautiana sana kutegemea majira na nususpishi. Idadi za kaskazini zilizo dogo zaidi ni nyeupe, hata hivyo idadi za kusini ni kubwa zaidi zenye manyoya ya rangi iliyoiva zaidi.

Pembeshada[hariri | hariri chanzo]

Jinsia mbili huzaa pembeshada (aina ya pembe ya spishi ya familia ya kulungu zinazogawanyika katika matawi) na spishi ya pekee ambayo majike huzaa pembe na pia madume.

Etimolojia[hariri | hariri chanzo]

Jina la "rangifer" ambalo Linnaeus alichagua kama jina kwa jenasi ya kulungu aktiki lilitumiwa na Albertus Magnus. Neno hili linaweza kutoka neno la Kilapi raingo.

Kwa Kiingereza, anaitwa reindeer yenye asili ya Kinorsi (Kinorsi cha Kale hreinn linatoka Kiproto-Kijerumaniki *hrainaz na Kiproto-Kihindi-Kizungu *kroinos linalomaanisha "mnyama mwenye pembe"). Kwa lugha za Kiurali, Kilapi poatsu (kwa Kilapi cha Kaskazini boazu, Kilapi cha Lule boatsoj, Kilapi cha Pite bâtsoj, kwa Kilapi cha Kusini bovtse), Kimari puča na Kiudmurti pudžej, majina yote hurejelea kulungu aktiki waliofungwa yanayotoka neno la Kiajemi *počaw kutoka Kiproto-Kihindi-Kizungu *peku- linalomaanisha "ng’ombe". Jina la Kifini poro pia linaweza kumaanisha "mchota-theluji" kwa tabia yake ya kuchota kupitia theluji ili kupata chakula. Kwa Kiinuktitut (lugha ya Kieskimo), karibuu (kulungu aktiki) anajulikana kwa jina la tuktu, kwa Kigrinlandi tuttu. Na kwa Kikrii-Montagnais-Naskapi karibuu anaitwa atihkw.