Korsika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Korsika
Mahali pa Korsika katika Ufaransa
Mahali pa Korsika katika Ufaransa

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Ufaransa Ufaransa
Mji mkuu Ajaccio
Eneo
 - Mkoa 278,650 km²
Tovuti: http://www.corse.fr/
Korsika

Korsika (Kifaransa:Corse; Kikorsika: Corsica) ni kisiwa cha Ufaransa katika Mediteranea. Ni kisiwa kikubwa cha nne katika Mediteranea baada ya Sisilia, Sardinia na Kupri.

Iko upande wa magharibi wa Italia na upande wa kusini ya Ufaransa na kaskazini ya kisiwa cha Sardinia. Umbali wa bara ni kilomita 90 hadi Italia na kkilomita 170 hadi Ufaransa ya kusini. Umbali na Sardinia ni 11 km pekee.

Kihistoria utamaduni wa watu wa Korsika ilikuwa karibu zaidi na Italia kuliko Ufaransa. Lugha ya Kikorsika iko karibu na lahaja za Italia. Leo ni takriban asilimia 35 za wakazi wanaotumia lugha hii. Serikali ya Ufaransa iliwahi kupigia marufuku matumizi yake mashuleni lakini tangu 1989 imekubaliwa kama lugha rasmi pamoja na Kifaransa.

Eneo la kisiwa ni 8680 km² zinazokaliwa na wakazi 278,650. Mji mkuu ni Ajaccio. Wilaya ni Corse-du-Sud na Haute-Corse.

Mwenyeji mashuhuri kabisa wa Korsika alikuwa Napoléon Bonaparte.

Kisiwa kina pwani lenye urefu wa kilomita 1,000 na milima mingi inayofikia kimo cha mita 2706.

Miji muhimu ni (majina ya Kikorsika)

Ajaccio (Aiacciu)
Bastia (Bastia)
Corte (Corti)
Sartène (Sartè)

Katika historia kisiwa kilikuwa chini ya Genua tangu mwaka 1300 hadi karne ya 18 kikauzwa kwa Ufaransa hivyo kuwa sehemu ya jirani ya kaskazini.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: