Nenda kwa yaliyomo

Jiografia ya Jibuti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Map of Djibouti
Satellite image of Djibouti, generated from raster graphics data supplied by The Map Library

11°30′N 43°00′E / 11.500°N 43.000°E / 11.500; 43.000

Jiografia ya Jibuti inalingana kwa karibu na ile ya mataifa mengine katika Mashariki mwa Afrika, Jibuti ilipo, ikipakana na Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamu, katikati ya Eritrea, Ethiopia na Somalia.

Kwa kilomita 13 Jibuti inapakana na Eritrea, huku kukiwa na urefu wa kilomita 337 za mpaka kati ya Jibuti na Ethiopia, na mpaka wa km 58 na Somalia Kwa ujumla ina mpaka wa km 506. Pia ina pwani ya urefu wa km 314. JIbuti inakaa kaika eneo la kufana, ikiwa karibu na leni zenye shughuli nyingi zaidi duniani la meli na pia karibu na mahali pa uchimbaji mafuta nchini Saudi Arabia.

Jibuti pia ni kituo cha reli katika reli ya Ethiopia-Jibuti.

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]

Hali yake ya anga ni ya joto kiasi, na pia haina mvua (ni jangwa).

Milima iliyopo katikati ya nchi hugawa tambarare za pwani kutoka plateau. Eneo la chini zaidi ni Ziwa Assal mita 155 chini ya usawa wa bahari na la juu zaidi ni volikano Moussa Ali yenye kimo cha mita 2028. Hakuna shamba la ukulima, unyunyizaji maji, mimea iliyojimeza huko (msitu upo tu katika milima ya Goda, hasa mbuga ya Day Forest). Takribani asilimia 9 ya nchi ni malisho yeliyojimeza (1993 mashariki). Kwa hiyo Jibuti inahesabiwa kuwa sehemu ya nyasi ya Ethiopia, isipokuwa kijisehemu kinachopakana na Bahari ya Shamu ambacho ni baadhi ya Jangwa la Pwani ya Eritrea ambayo inajulikana kuwa njia nzuri ya uhamiaji wa ndege ambao wanaweza kuwindwa[1].

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Matukio ya kimaumbile ni pamoja na Matetemeko ya ardhi, kiangazi, mawimbi kutoka Bahari ya Hindi ambayo husababisha mafuriko na mvua kubwa. Malighafi ni pamoja na umeme kutoka ardhini (geothermal energy). Eneo hili limekumbwa na uhaba wa maji salama ya kunywa na pia kugeuka kwa eneo hilo kuwa jangwa.

Jibuti ni mwanachama wa makubaliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ueneaji wa jangwa, viumbehai vilivyo hatarini, sheria ya bahari, kulinda ukanda wa ozoni na uharibifu wa mazingira na meli.

Ukubwa wa Eneo

[hariri | hariri chanzo]
jumla: km2 23000
ardhi: km2 22980
maji: km2 20

Madai ya maji ya kitaifa

[hariri | hariri chanzo]
contiguous zone: nmi 24
eneo la kiuchumi pekee: nmi 200
Bahari ya mpaka: nmi 12
Topografia ya Jibuti