Ziwa Assal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa ziwa lenye jina la karibu angalia Assale (Ethiopia)

Ziwa Assal
Mahali Bonde la Afra
Aina ya ziwa Ziwa la Crater
Mito ya kuingia chini ya ardhi kutoka bahari
Mito ya kutoka hakuna
beseni 900 km2
Nchi za beseni Jibuti
Urefu 10 km
Upana 7 km
Eneo la maji 54 km2
Kina cha wastani 7.4 m
Kina kikubwa > 20 m
Mjao 400 million m3
Kimo cha uwiano wa maji uso juu ya UB -155 m
Miji mikubwa ufukoni Randa 25 km Kaskazini-Mashariki)

Ziwa Assal (far. Lac Assa) ni ziwa la chumvi lililopo nchini Jibuti. Liko katika mpaka wa kusini wa mkoa mwa Tadjoura, ikiguza eneo la mkoa wa Dikhil, takribani 120 km magharibi mwa Mji wa Jibuti. Iko 155 m chini ya usawa wa bahari katika Bonde la Afar. Fuo zake zinashirikisha eneo la chini zaidi barani Afrika na ni ya pili ya chini zaidi duniani baada ya Bahari ya Chumvi huko Palestina. Urefu wake mkubwa unafikia kilomita 19 na upana wake mkubwa hadi km 7; eneo la maji yake ni hadi km² 54. Kina cha juu kinafikia hadi mita 40. Beseni yake inajumlisa maeneo ya km² 900.

Ziwa hili halina njia ya kutoka kwa maji isipokuwa uvukizaji. Tokeo lake ilhali maji ya kuingia yana kiasi cha chumvi ndani yake ya kwamba kiwango cha chuumvi katika maji ya ziwa kinazidi kuongezeka. Leo hii ni ziwa lenye chumvi nyingi duniani [1] kushinda Bahari ya Chumvi.

Eneo la ziwa hili ni kama jangwa na hakuna fauna au flora ionekanayo katika mimea midogo katikati ya Ziwa hilo.

Kipimo cha juu cha joto katika eneo hilo hufanya maji kugeuka ukungu kwa urahisi, kwa hivyo eneo hilo limezungukwa na mwamba wa chumvi iliyoshikamana.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Kiini[hariri | hariri chanzo]

  1. isipokuwa maziwa machache kwenye bara la Antaktika yaliyopimiwa kuwa na chumvi zaidi