Yordani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jordan)
Ufalme wa Kihashemi wa Yordani
المملكة الأردنية الهاشمية
Al-Mamlakah al-Urduniya al-Hāšimiya
Bendera ya Yordani Nembo ya Yordani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}}
Wimbo wa taifa: عاش المليك
' ash al-malik   
"Heri kwa mfalme"
Lokeshen ya Yordani
Mji mkuu Amman
31°57′ N 35°56′ E
Mji mkubwa nchini Amman
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Ufalme wa Kikatiba
Abdullah II
Bisher Al-Khasawneh
Uhuru
Tarehe

25 Mei 1946
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
89,342 km² (ya 112)
0.8
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - 2015 sensa
 - Msongamano wa watu
 
10,407,793 (ya 86)
9,531,712
114/km² (ya 70)
Fedha Dinar ya Yordani (JOD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UTC+2 (UTC+2)
UTC+3 (UTC+3)
Intaneti TLD .jo
Kodi ya simu +962



Yordani (pia: Jordan, Jordani; kwa Kiarabu; الأردنّ "al-urdun") ni ufalme wa Kiarabu katika Mashariki ya Kati.

Jina la nchi limetokana na mto Yordani ambao ni mpaka wake upande wa magharibi na Israel na eneo la Palestina ya leo.

Jina rasmi ni Ufalme wa Kihashemi wa Yordani (kwa Kiarabu: المملكة الأردنية الهاشمية ) kutokana na familia ya kifalme.

Imepakana na Syria, Iraq, Saudi Arabia, Palestina na Israeli.

Ina pwani fupi kwenye Ghuba ya Aqaba ya Bahari ya Shamu.

Mji mkuu ni Amman.

Jiografia

Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa.

Bahari ya Chumvi ina kiwango kikubwa cha chumvi, kiasi kwamba watu wanaweza kuelea juu yake bila juhudi yoyote.

Historia

Nchi ya sasa ilianzishwa kwa jina la "Transjordan" (ng'ambo ya mto Yordani) kama sehemu ya eneo la Palestina lililotawaliwa na Uingereza kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa baada ya mwaka 1918.

Waingereza waliamua kutenganisha eneo hilo na Palestina upande wa magharibi wa mto Yordani na kuiweka tangu mwaka 1921 chini ya mamlaka ya Abdullah bin al-Husayn wa familia ya Wahashemi aliyekuwa mtoto wa Sharif wa Makka wa mwisho kabla ya mji huu kutwaliwa na Wasaudi.

Kwa hatua hiyo Uingereza ililenga kuimarisha uhusiano wake na makabila ya Waarabu wa jangwa. Abdullahi alitawala awali kwa cheo cha emir baadaye kama mfalme wa "Transjordan".

Jeshi lake lilishiriki katika vita ya mgawanyo wa Palestina na Israeli miaka 1948-1949 na kushika sehemu ya Palestina isiyotawaliwa na Israeli.

Baada ya vita ya siku sita ya mwaka 1967 maeneo yote upande wa magharibi wa mto Yordani yaliyotawaliwa na mfalme Hussein II mwandamizi wa Abdallah tangu mwaka 1952.

Mwishowe aliacha madai yote ya utawala juu ya sehemu hizo.

Sehemu ya kambi ya Zaatari yenye wakimbizi 80,000 kutoka Syria.

Watu

Wenyeji walio wengi (95-97%) ni Waarabu wenye undugu mkubwa kijenetikia na Waashuru Wakristo ambao ni 0.8%.

Kuna umati wa wakimbizi kutoka Palestina (ingawa wengi wamepata uraia) na miaka ya mwisho kutoka Iraki na Siria. Wageni wote ni 30% za wakazi.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu.

Upande wa dini, 95% ni Waislamu (karibu wote Wasuni), 4% ni Wakristo (hasa Waorthodoksi na Wakatoliki), 1% ni Wadruzi na wachache ni Bahai.

Tazama pia

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yordani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.