Amman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Amman - عمان
Amman.jpg
Amman nchini Yordani
Habari za kimsingi
Mkoa Mkoa wa Amman
Anwani ya kijiografia Latitudo: 31º57'00" N - Longitudo: 035º 55' 59" E
Kimo 773 m juu ya UB
Eneo ?? km²
Wakazi milioni 1.5
Msongamano wa watu watu ?? kwa km²
Simu +962 (nchi), 6 (mji)
Mahali
Jo-map.jpg

Amman (kar.: عمان ʿammān) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Yordani mwenye wakazi milioni moja na nusu au zaidi mjini na angalau milioni mbili na nusu katika rundiko la mji.

Msikiti wa Mfalme Abdullah

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mji uko takriban km 40 kutoka ncha ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi kati ya vilima vya Yordani ya kaskazini-magharibi. Hali ya hewa ni afadhali kushinda mahali pengi pa Yordani kwa sababu ya kimo cha mji hivyo joto halizidi mno.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Amman ni mji mwenye historia ndefu iliyojulikana kwa jina la Rabat Amon wakati wa Biblia. Ilistawi vizuri hadi nyakati za Dola la Roma ilipopambwa na majengo makubwa na mazuri yanayoonekana hadi leo. Lakini umuhimu wake ulipungua siku za Wamuawiya na wakati wa kuundwa kwa Yordani palikuwa na kijiji tu. Mfalme Abdullah bin al-Husayn alianzisha hapa mji mkuu wake. Hadi vita kuu ya pili ya dunia Amman haikuzidi wakazi 30,000.

Lakini mji ulikua haraka baada ya kuundwa kwa Israel kwa sababu wakimbizi wengi kutoka sehemu za Palestina zilizokuwa Israel walikaa Amman.

Kipindi cha pili cha kukua kilitokea tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Lebanoni wakati wa miaka ya 1975-1990. Sehemu kubwa ya mabenki na biashara kutoka Beirut vilihamia Amman iliyoendelea kuwa kitovu kipya cha biashara na uchumi upande wa mashariki ya Mediteranea.

Picha za Amman[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Map of Asian states.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Amman kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.