Milima ya Udzungwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Milima ya Udzungwa

Milima ya Udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana katika bara la Afrika, nchini Tanzania, mkoani Morogoro, wilaya ya Kilombero.

Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi.

Jina la hifadhi limetokana na milima hiyo ya Udzungwa ambayo ndani yake kuna makazi ya wanyamapori wa aina mbalimbali.

Ina ukubwa wa kilometa mraba 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani.

Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee: "Mbega Mwekundu wa Iringa" (Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka 1979.

Aina nyingine nne za ndege ambao hazikufahamika hadi miaka ya karibuni ni: chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya iliyogunduliwa ya kwale wa Udzungwa zinazofanya hifadhi hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika.

Pia Mto Sanje ni kivutio kikubwa sana. Mto huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.

"African violet" ni ua ambalo linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya miti mirefu inayofikia mita 30.

Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, chui, nyati na tembo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]