Nenda kwa yaliyomo

Muammar al-Gaddafi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muammar al-Gaddafi
al-Gaddafi mwaka 2006
al-Gaddafi mwaka 2006
Kiongozi wa mapinduzi
Tarehe ya kuzaliwa 1942
Mahali pa kuzaliwa Sirte
Tarehe ya kifo 20 Oktoba 2011
Alingia ofisini 8 Septemba 1969
Alitanguliwa na Mfalme Idris I wa Libya
Dini Uislamu


Amiri Muammar al-Gaddafi (kwa Kiarabu:معمر القذافي Mu‘ammar al-Qadhāfī) alikuwa kiongozi wa taifa la Libya.

Maisha

Alizaliwa katika familia ya mabedawi (wafugaji wa kuhamahama) mnamo mwaka 1942.

Baada ya masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Libya alijiunga na jeshi mwaka 1963 akasoma kwenye chuo cha kijeshi cha Sandhurst (Uingereza) mwaka 1965.

Tarehe 1 Septemba 1969 pamoja na maafisa wenzake alipindua serikali ya mfalme Idris I na kutangaza Jamhuri ya Kiarabu ya Libya.

Ingawa hakuwa na cheo rasmi aliendelea kutawala nchi yake akiitwa "Kiongozi wa mapinduzi ya 1 Septemba ya Jamahiriya ya Ujamaa ya watu ya Kilibya-Kiarabu".

Hatimaye akapinduliwa mwenyewe tarehe 23 Agosti 2011, na kuuawa tarehe 20 Oktoba 2011.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muammar al-Gaddafi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.