Kiranja Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiranja Mkuu au Mkuu wa viranja (pia: Kaka mkuu ama Dada mkuu; kwa lugha ya Kiingereza "Head Prefect"; kifupi: "HP") ni kiongozi wa serikali ya wanafunzi shuleni, hasa katika shule ya msingi na sekondari.

Kiranja ni mwanafunzi aliyechaguliwa na walimu au wanafunzi wenzake kwa lengo la kuwasimamia usafi, nidhamu, mazingira ya wanafunzi na kuweka daraja kati ya waalimu na wanafunzi.

Kiranja Mkuu ndiye anayewasimamia na kuwaagiza viranja wengine, ni kama Rais na wizara zake.

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiranja Mkuu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.