Muhimbili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Muhimbili ni mahali maarufu jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla, hasa kutokana na hospitali na chuo kikuu vinavyopatikana huko. Ipo barabara ya Umoja wa Mataifa mtaa wa Upanga Magharibi.[1]

Jina Muhimbili limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.

Chuo kikuu cha Muhimbili kilianzishwa mwaka 1963: kilifunguliwa kama "Chuo cha Afya Dar es Salaam" ndani ya hospitali iliyoitwa awali Princess Margaret Hospital na wanafunzi 10 waliofuata kozi za uganga au upasuaji.

Mwaka 1968 kikafanywa ni kitengo cha tiba katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tangu 2007 imeandikishwa kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (kwa Kiingereza: Muhimbili University of Health and Allied Sciences; kifupi: MUHAS[2]).

Leo hii Muhimbili ina shule ya madaktari, wauguzi, mafamasia, waganga wa meno, maafisa afya mazingira, maafisa mazingira na elimu ya juu ya afya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Chuo Kikuu cha Muhimbili (2017). Historia ya chuo kikuu cha Muhimbili.
  2. Chuo Kikuu cha Muhimbili | Chuo Kikuu cha Muhimbili. www.muhas.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-11-06.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]