Aishi Manula
Aishi Salum Manula, alizaliwa 13 Septemba 1995 ni mchezaji wa Simba S. C anacheza kama mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Tanzania[1]. Na pia amewahi kuchezea timu nyingine kadhaa, zikiwemo Azam fc, kwa sasa yupo anacheza timu ya Simba SC.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Manula alizaliwa nchini Tanzania katika Mkoa wa Morogoro na wakati wa ujana alianza kazi yake katika klabu ya soka ya Mkamba rangers iliyopo wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.
Katika mwaka 2012 alijiunga na Azam F.C akiwa na umri wa miaka 17 tu, ushindi wake na ushirikiano wake umemsaidia kucheza katika kikosi cha kwanza hadi mkataba wake ulipofikia mwisho.
Baada ya mafanikio ya kuvutia na Azam FC katika Ligi Kuu ya Tanzania vilabu vingi vilikuwa vinakaribia nafasi ya kumsaini. Uvumi wa kusaini ulifanya vyombo vya habari viseme juu ya Aishi kununuliwa na klabu mbalimbali na hatimaye kujiunga na Simba S.C. mwaka 2017 ambapo anaendelea kufanikiwa kwenye ligi na kusaidia timu yake kuchukua kikombe cha ligi na yeye mwenyewe akichukua glovu ya dhahabu.
Aishi Manula anashikilia rekodi ya kutwaa tuzo za kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo: mara mbili ameitwaa akiwa na Azam FC na mara mbili akiwa na Simba SC.
Aishi Manula ana rekodi ya kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika akiwa na Simba na kufika hatua ya Robo Fainali.
Pia kipa huyu ameisaidia Tanzania kushiriki michuano ya Afcon mwaka 2019 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aishi Manula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |