Wilaya ya Mbulu

Wilaya ya Mbulu ni wilaya moja ya Mkoa wa Manyara. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Mbulu ilihesabiwa kuwa 320,279 waishio humo. [1]
Mbulu imepakana na Mkoa wa Arusha pamoja na ziwa Eyasi upande wa kaskazini, wilaya ya Babati Vijijini upande wa mashariki, wilaya ya Hanang upande wa kusini na mkoa wa Singida kwa magharibi.
Wenyeji asilia ni hasa Wairaqw (Wambulu).
Mwaka 2015 wilaya iligawiwa kwa Wilaya ya Mbulu Mjini na Wilaya ya Mbulu Vijijini.
Makao makuu iko Mbulu mjini na mji huu ulianzishwa kama kituo cha Wamisonari wa Afrika wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa jina la Neu-Trier.
Mwaka 2018 iliamuliwa kujenga ofisi mpya kwa ajili ya Wilaya ya Mbulu Vijijini katika kata ya Haydom[2].
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Sensa ya 2012, Manyara Region – Mbulu District-Council
- ↑ "Halmashauri ya Mbulu kuhamiwa Hydom", gazeti la Mwananchi, toleo la 28 Machi 2018, uk. 34
![]() |
Kata za Wilaya ya Mbulu - Mkoa wa Manyara - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Ayamaami | Ayamohe | Bargish | Bashay | Daudi | Dinamu | Dongobesh | Endagikot | Endamilay | Eshkesh | Gehandu | Geterer | Gidihim | Gunyoda | Hayderer | Haydom | Imboru | Kainam | Maghang | Marang | Maretadu | Masieda | Masqaroda | Murray (Mbulu) | Nahasey | Nambisi | Sanu Baray | Tlawi | Tumati | Uhuru | Yaeda Ampa | Yaeda Chini |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mbulu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|