Kiburumo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala yenye habari za kimdomo bila vyanzo halisi

Makala hii (au sehemu zake) inaonekana kutoa habari za kimdomo kuhusu desturi au utamaduni wa maeneo ya Tanzania. Hailingani na masharti ya kuonyesha vyanzo na ushuhuda wa kimaandishi jinsi ilivyo kawaida katika Wikipedia.

Lakini ilhali habari nyingi katika mazingira yetu hazikuandikwa bado wala kujadiliwa kimaandishi na wataalamu tunaacha habari hizi kwa muda. Tunaomba wasomaji wetu kuwa macho na kutochanganya habari hizi za kisimulizi na habari zenye ushuhuda halisi. Tunaendelea kuangalia michango ya aina hii ambayo haiwezi kukubaliwa jinsi ilivyoletwa kama inapingana na ushuhuda halisi..

Kiburumo ni kijiji kinachopatika katika kata ya Selembala, tarafa ya Mvuha, Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoa wa Morogoro.

Kijiji hicho kina vitongoji vitatu navyo ni Viduari, Mikoroshini na Sinza. Kwa jumla kina kaya 700, shule ya msingi moja na zahanati moja.

Kabila la wenyeji ni Wakutu, ila kutokana na mwingiliano wa watu sasa yapo makabila tofauti. Koo maarufu ni Ndago, Mzenga, Manyire, Kitogota, Pazi, Mparangiru, Mnemo, Makinda, Mkuyu n.k.

Shughuli ya uchumi ni kilimo cha ufuta na tumbaku. Kilimo cha chakula ni mahindi, mtama, kunde na maharage.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kiburumo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.