Nenda kwa yaliyomo

Tikitimaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tikitimaji.
shamba la mitikiti-maji huko jangwa la Kalahari.

Tikitimaji au tikiti-maji ni tunda la mtikiti-maji lenye maji na nyama ambalo huchangia kutoa ngazi ya juu ya vitamini, madini n.k. Matikitimaji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hiyo inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama matango, maboga na maskwash.

Kilimo cha matikitimaji[hariri | hariri chanzo]

Tikitimaji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani.

Zao hili linawapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Zao la tikitimaji ni mojawapo ya mazao ambayo yana faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.

Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekari moja (1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha tani 15-36, ambacho kitampatia fedha zitakazomsaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na umaskini.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wastani yaani haihimili hali ya joto kali sana, baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota.

Upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakteria ambayo huathili mavuno.

Faida za tikiti-maji[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tikitimaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.