Nenda kwa yaliyomo

Jangwa la Kalahari

Majiranukta: 23°S 22°E / 23°S 22°E / -23; 22
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jangwa la Kalahari (lililoonyeshwa kwa rangi nyekundu nyeusi) na Beseni la Kalahari (rangi ya chungwa).
Kalahari huko Namibia.

Kalahari ni eneo kubwa lenye tabianchi yabisi na nusu yabisi kusini mwa Afrika lenye kilomita za mraba 900,000 hivi katika Botswana na sehemu za Namibia na Afrika Kusini.

Ni tofauti na jangwa la Namib lililopo nyuma ya pwani ya Atlantiki ya Namibia na Angola.

Jina "Kalahari" linatokana na neno la Kitswana "Kgala", linalomaanisha "kiu kubwa" au kutoka "Kgalagadi" inayomaanisha "pasipo maji". Kalahari ina maeneo makubwa yaliyofunikwa na mchanga tu bila maji ya kudumu.

Kalahari huwa na wanyama na mimea kadhaa kwa sababu sehemu kubwa si jangwa kabisa. Kuna kiasi kidogo cha mvua. Majira ya joto ni makali sana. Maeneo yenye ukavu zaidi huwa na milimita 110-200 za mvua kwa mwaka. Maeneo yenye usimbishaji mkubwa zaidi huwa na milimita 500.

Makorongo makavu ya mito ya zamani yanapatikana kaskazini mwa Kalahari, yakijaa maji wakati wa mvua na yanayobaki kama mabwawa madogo kwa miezi kadhaa.

Beseni la Kalahari

[hariri | hariri chanzo]

Beseni la Kalahari ni pana zaidi likikusanya maji yote yanayotiririkia mle kwenye eneo la km2 milioni 2.5. Beseni hilo huenea hadi Botswana, Namibia na Afrika Kusini, pamoja na sehemu za Angola, Zambia na Zimbabwe.

Kuna mto mmoja wa kudumu pekee ambao ni mto Okavango. Okavango inaishia katika delta ya ndani inayofanya sehemu za vinamasi vyenye wanyamapori wengi.

Sehemu kubwa ya jangwa nchini Botswana imekuwa sehemu ya Hifadhi ya Kalahari ya Kati.


Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Main, Michael (1987). Kalahari : life's variety in dune and delta. ISBN 1868120015.

Kigezo:Commons and category

23°S 22°E / 23°S 22°E / -23; 22