Ukavu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dhoruba ya vumbi inatokea penye ukavu mkubwa kwa muda mrefu

Ukavu ni hali ya kukauka, pasipo na unyevu au maji kwa hali ya kiowevu au mvuke. Ilhali viumbe vyote duniani hutegemea kuwepo kwa maji, ukavu si mazingira yanayoruhusu kustawi kwa uhai.

Jangwa ni mazigira kavu, na ukavu wake yaani ukosefu wa maji husababisha kupotea kwa mimea na wanyama wengi. Wale waliopo wana maumbile yanayolingana na ukavu, yakitunza unyevu mwilini na kufanya shughuli zao hasa usiku ambako joto linapungua.

Maji yanapatikana pia kwa hali ya ukavu kama ni barafu au theluji kwenye hali ya jalidi kali. Wachezaji wa skii hupendelea theluji kavu kuliko theluji bichi inayopatikana wakati halijoto inakaribia °C 0.

Ukavu hufanya tofauti kati ya vumbi na matope. Dhoruba ya vumbi hutokea katika mazingira penye maeneo makavu sana.