Nenda kwa yaliyomo

Skii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Skii asilia: Wasami katika Skandinavia wakati wa karne ya 18
Aina mbalimbali ya skii zinazotumiwa mlimani
Kuruka mbali kwa skii
Skii za mbio kwenye tambarare

Skii au relitheluji ni ubao mrefu na mwembamba unaofungwa chini ya kiatu kwa kusudi la kutelezea kwenye theluji.

Chanzo cha skii[hariri | hariri chanzo]

Vifaa hivi vilianzishwa na mataifa yaliyoishi katika mazingira ya baridi ambako mara kwa mara uso wa nchi hufunikwa kwa theluji.

Ilhali theluji inaweza kufunika uso wa nchi kwa unene wa sentimita au hata mita kadhaa si rahisi kutembea juu yake kwa sababu mguu unaweza kuzama ndani ya theluji kwa kila hatua ambayo inachelewesha mwendo na kuchosha.

Kufunga skii mguuni kunaleta faida mbili:

  • uso mkubwa wa skii huzuia kuzama chini ndani ya theluji
  • uso nyororo wa skii unaruhusu kuteleza juu ya theluji kwa kasi kubwa kuliko kukimbia kwenye nchi kavu.

Etimolojia na historia[hariri | hariri chanzo]

Asili ya jina "skii" iko katika Kinorwei cha kale.[1] [2] Matamshi yake kwa kawaida ni "shi".

Mifano ya kale ya skii imepatikana kutoka Urusi, Uswidi na Norwei ambayo umri ulioweza kuthibitishwa watu walianza kutumia vifaa hivi miaka 8,000 iliyopita.

Teknolojia ya skii iliendelezwa mwanzoni ma karne ya 20 katika nchi za Skandinavia kwa shabaha ya kumwezesha mtumiaji kupiga kona haraka zaidi. Maendeleo yalihusu hasa namna ya kufunga mguu kwenye ubao na pia matumizi ya plastiki badala ya ubao, pamoja na kubuni mabuti ya pekee kwa matumizi pamoja na skii.

Mabadiliko hayo yaliendeshwa hasa na wanamichezo waliokuta skii kwa watumiaji wake wa kiasili na kuipeleka kwa nchi nyingine kwa kusudi la burudani na mashindano.

Utengenezaji[hariri | hariri chanzo]

Skii imeibuka kutoka kujengwa kwa ubao mgumu uliochongwa. Baada ya kuenea kwa michezo ya skii katika Ulaya ubao mgumu ulikuwa haba na ghali, hivyo mafundi walianza kuunganisha aina mbalimbali za ubao.

Tangu kupatikana kwa plastiki mata hii imetumiwa pia kwa kutengeneza skii. Kwa mashindano ya hali ya juu kuna pia skii zinazotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya juu ya kaboni.

Aina za skii[hariri | hariri chanzo]

Skii hutengenezwa tofauti kulingana na matumizi yake.

  • Skii za kuruka hutumiwa na wanamichezo wanaoteleza mlimani hadi ngazi wanapolenga kuruka mbali iwezekanavyo hadi kutua; umno ni pana na ndefu
  • Skii za mbio wa mlimani zinafaa kwa kupiga kona mara nyingi na kufikia kasi kubwa ya zaidi ya km 100 kwa saa; mi fupi na nyembamba
  • Skii za mbio au matembezi ya mbali hutumiwa na wanamichezo na pia watu wanaozitumia kwa burudani; hazifai kwa mitelemko mikali; ni nyembamba na ndefu

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Merriam-Webster's Dictionary
  2. Aasen, Ivar (1950): Ordbog over det norske Folkesprog. Kristiania: Carl C. Werner.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]