Hifadhi ya Kalahari ya Kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Twiga wa Afrika ya Kusini

Hifadhi ya Kalahari ya Kati (Central Kalahari Game Reserve) ni mbuga kubwa ya wanyamapori katika jangwa la Kalahari la Botswana. Ilianzishwa mwaka 1961 kwenye eneo la kilomita za mraba 52,800, ambazo ni takribani asilimia 10 za Botswana yote. Hivyo ni hifadhi ya wanayamapori ya pili duniani kwa ukubwa. [1]

Hifadhi ina wanyamapori kama vile twiga, tembo, kifaru cheupe, nyati, fisi madoa, fisi kahawia, cheche, nguchiro, ngiri, duma, simbamangu, mbwa mwitu, bweha, chui, simba, nyumbu, punda milia, pofu, choroa, tandala, impala, mhanga, na mbuni.

Eneo hili ni hasa tambarare, likiinuka na kushuka kidogo. Uoto ni vichaka, nyasi na miti kwenye maji ya kutosha.

Wakazi asilia ni Wasan walioendesha hapa maisha ya wawindaji bila makazi ya kudumu. Tangu miaka ya 1990 serikali ya Botswana ilianza kuhamisha Wasan nje ya hifadhi na ni 250 pekee wanaobaki. [2] Sheria zinazokataza uwindaji nchini ni kikwazo kikubwa kwa Wasan kuendelea na utamaduni na maisha yao. [3]

Mnamo mwaka 2014 mgodi wa almasi ulianzishwa katika sehemu ya kusini mashariki mwa hifadhi hiyo. Kampuni ilikadiria kuwa mgodi huo unaweza kutoa almasi yenye thamani ya dola bilioni 4.9. Ripoti ya Rapaport Diamond, mwongozo wa bei ya tasnia ya almasi, alisema, "Uzinduzi wa Ghaghoo haukuwa na ubishi [...] kutokana na eneo lake kwenye ardhi ya mababu ya Wabushini". [4]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Central Kalahari Game Reserve - Attractions - Tourism of Botswana". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-05. Iliwekwa mnamo 2011-05-05.
  2. "Go2Africa.com". Go2Africa.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-05. Iliwekwa mnamo 2013-09-24.
  3. "In Botswana reserve, Bushmen still being deprived of rights". 
  4. Miller, Jeff (5 Septemba 2014). "Gem Diamonds Opens Its Underground Ghaghoo Mine". Rapaport | Diamonds.Net.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]