Nyegere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nyegere
Honey badger.jpg
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Mustelidae (Wanyama walio na mnasaba na chororo)
Jenasi: Mellivora
Storr, 1780
Spishi: M. capensis
(Schreber, 1776)

Nyegere, melesi au mhilu (Mellivora capensis) ni mnyama mdogo wa familia Mustelidae anayetokea Afrika, Mashariki ya Kati na Uhindi.

Nyegere huishi peke yao kwenye shimo analolichimba yeye mwenyewe. Ni wachimbaji wazuri sana. Vile vidole vyao vyenye kucha ndefu na ngumu humsaidia sana kwenye kazi hii. Hata kama ardhi ni ngumu sana, ana uwezo wa kuchimba shimo linalomtosha kujificha katika kipindi kinachokadiriwa kuwa ni dakika kumi tu.

Crystal Clear app babelfish.png Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyegere kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.