Majadiliano:Nyegere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nyegere ni Mnyama mdogo jamii ya paka au Komba, Kwa Tanzania hupatikana zaidi Kanda ya kaskazini hasa sehemu za Milima ya Kamwala wilayani Mwanga-Kilimanjaro. Pia hupatikana kanda ya ziwa Mara-Musoma,Bunda na Serengeti Mwanza- Sehemu za Sumve na Misungwi. Kuna aina mbalimbali za Nyegere, katkaka mazingira yetu aina mbili ndizo zinapatikana kwa wingi. Yakwanza ni wale weusi mwili wote na aina ya pili ni wale wenye weupe katika mikia yao hasa katika ncha ya mkia.

Nyegere hua katika utafutaji wa chakula wakati wa usiku zaidi ni vigumu kumkuta nyegere akiwa anazurura wakati wa mchana, wakati wa mchana anakua katika pango au sehemu za vichaka. Nyegere hupendelea kula kuku na ni tatizo kubwa sana kwa wafugaji wa kuku hasa wale wanaofuga kwa kuwaachia kuku huru, ufugaji horera.

Nyegere ni Mnyama mkali japo mdogo kwa umbo, Nyegere anapokasirishwa maranyingi lazima afanye kitu kibaya kwa manadamu kama utashindwa kumuwahi na kumdhibiti( kwa lale wanaotokea Kilimanjaro hasa milima ya Upareni-Kamwala mwanga anajilikana kama MBA)

Inasemekana kua MBA-Nyegere anapokutana na mwanaume hukimbilia kung'ata sehemu za siri (Mapumbu), na mwanamke hukimbilia Matiti. Japo kwangu mimi sijawahi kukutana na kesi kama hiyo ya mtu aliyepata tatizo la kung'atwa matiti au mapumbu.

Wako katika kuelimishana Hassani Badi Chaula

Weka matini yako katika makala[hariri chanzo]

Hassani (na Mwandikaji) salaam. Majadiliano si mahali pa kuandika matini ya makala. Makala ya Nyegere imeshaandikwa. Lakini unaweza kuichangia ukiwa na taarifa nyingine au ukiona makosa. ChriKo (majadiliano) 19:44, 21 Desemba 2015 (UTC)