Mbuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbuni
Mbuni Somali
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Struthioniformes (Ndege kama mbuni)
Familia: Struthionidae (Ndege walio na mnasaba na mbuni)
Jenasi: Struthio
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 2, nususpishi 4:

Msambao wa mbuni katika Afrika
Msambao wa mbuni katika Afrika

Mbuni ni ndege wakubwa wa familia Struthionidae. Kuna spishi mbili katika jenasi moja, lakini wataalamu wengine wanafikiri ni spishi moja tu. Ndege hao ni wakubwa kuliko wengine wote. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na wanaweza kukimbia sana, hata kwa mwendo wa km 65 kwa saa, lakini hawawezi kuruka hewani.

Rangi za manyoya ya dume ni nyeusi na nyeupe na rangi ya ngozi yake (shingo na miguu) ni nyekundu, pinki au buluu kufuatana na nususpishi. Manyoya ya jike ni kahawiakijivu na rangi ya ngozi ni sawa na dume. Mbuni wanaishi katika savana, nyika na majangwa ya Afrika, lakini wanafugwa ulimwenguni mwote.

Jina la kisayansi la spishi kuu, Struthio camelus, linatoka katika lugha ya Kiyunani: στρουθιον = jurawa na καμηλος = ngamia.

Dume la mbuni ana harimi ya majike 2-7 lakini moja tu anatawala. Dume hupanda majike yote ya harimi yake na majike huyataga mayai yao yote katika tago moja ambalo dume amelitengeneza. Jike anayetawala hutaga kwanza na baadaye hutupa mayai ya majike wasio na nguvu sana. Kwa kawaida hubakisha mnamo mayai 20. Majike huyaatamia mayai mchana na dume hufanya usiku, kwa sababu rangi ya jike inafanana na mchanga na rangi nyeusi ya dume haionekani usiku.

Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

Mbuni ni ndege wakubwa, huku asili yao ikiwa ni Afrika. Hawa ni ndege wasio na uwezo wa kuruka. Wanapatikana kwenye oda ya Struthioniformes, pamoja na ndugu aitwaye kiwi. Mbuni ni wa pekee sana sababu ya muonekane wake, wa shingo na miguu mirefu pamoja na uwezo wake mkubwa wa kukimbia, karibu ya maili 45 kwa saa. Huu ni mwendokasi mkubwa zaidi kwa ndege yeyote ardhini. Mbuni ndiyo ndege mkubwa kuliko wote wanaoishi duniani, wakiwa pia ndio watagaji wa mayai makubwa kuliko wote pia.

Mlo wa mbuni kwa kiasi kikubwa huwa ni mimea, ingawa pia hula wadudu. Mbuni huishi katika makundi ya kutansatanga kati ya ndege watano mpaka hamsini. Wanapotishwa, mbuni hujificha kwa kulala ardhini au kukimbia mbali kama wakizingirwa, hushambulia adui zao kwa miguu yao yenye nguvu. Tabia kujamiiana hutofautiana kutoka maeneo moja mpaka vingine, ambapo mbuni dume hupigaia mbani jike hupigania nafasi ya kuwapata mbuni jike kwa nguvu.

Mbuni hufugwa dunia nzima, hasa kutokana na manyoya yake, ambayo hunitia na kutumika kuondolea vumbi. Ngozi yake hutumika kutangenezea mtu mbali mbali huku nyama yake ikilizwa kibiashara.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Mbuni huwa na uzito wa kilogramu 63-130, luku mbuni dume wakifika mpaka uzito wa kg 155. Manyoya ya mbuni dumu wakubwa huwa kwa kiasi kikubwa meusi huku mkia ukiwa wakubwa huwa na rangi ya kahawia na nyeupe. Vichwa vya mbuni wote huwa havina manyoya. Ngozi za mbuni jike huwa na rangi ya pinki – kijini, huku dume wakiwa na ngozi ya bluu au kijini kutegemeana na nususpishi.

Shingo zao ndefu, hukiweka kichwa chao mita 1.8 mpaka 2.75 juu ya ardhi, na macho yao husemwa kuwa ndiyo makubwa kuliko wanyama wote wa ardhini, yakiwa na sm 5, hivyo huweza kuwaona adui zao hata wakiwa mbali sana. Macho yao yanakingwa na mwanga mkali wa jua kutoka juu.

Miguu ya mbuni, kama ilivyo kwa ndege wengine, haina manyoya isipokuwa magamba. Ndege hawa wawili huwa na vidole vikubwa viwili huku wengi wakiwa na vine, huku kucha moja ikiwa kubwa, ikifanana na kwato. Mbawa hutanuka kwa upana wa mita 2 hivyi, na hutumika sana kwenye tabia za kujamiiana na kujikinga na jua. Wana manyoya 50-60 hivi ya mkiani. Midomo yao huwa mipana na ncha ya duara kidogo. Tofauti na ndege wengine, mbuni hutoa mkoja tofauti na kinyesi, hivyo kuwa na kibofu. Pia tofauti na ndege wengine tena, huwa na ogani ya kutolea manii inayoweza kutoka nje ya mwili kwa urefu wa inchi 8.

Mbuni hukomaa na kuwa na uwezo wa kuzaa wakiwa na miaka miwili/minne watoto wa mbuni hukua kwa kiasi ya sm 25 kwa mwezi. Wakiwa na umri wa mwaka mmoja tu, mbuni huwa na uzito wa kg 45. Mbuni jike huweza kuyatambua mayai yake hata kwenye kiota cha jumuiya.

Uzazi[hariri | hariri chanzo]

Mbuni wakipapatika

Kujamiiana huwa na misimu tofauti kutokana na maeneo. Mbuni dume hupigania nafasi ya kujamiiana na jike wengine, na akishinda basi huwa na uwezo wa kujamiiana na jike wote wa kundi lake lote japo atakuwa na jike wake atakayedumu naye kwa wakati husika.

Mbuni dume humvutia mbuni jike, kwa kumchezeachezea na kumpigia mbawa zake, ambaye humfuata na wao huenda faragha kwa ajili ya kujamiiana. Wakifika huko huwafukuza wanyama/mbuni wengine kama wapo na kisha dume kuweza tena, mbuni jike hukaa chini na kuwa tayari kwa kujamiiana.

Mbuni jike hutaga mayai yaliyorutubishwa kwenye kiota cha jumuiya, ambacho huwa ni shimo lenye upana wa mita tatu na kina cha sentimeta 30-60. Mbuni dume ndiyo huchimba kiota hiki mayai ya mbuni ndiyo mayai makubwa kuliko yote na huwa na uzito wa kg 1.4, zaidi ya mara 20 ya yai la kuku. Huwa na rangi ya maziwa na wakati mwingine pamoja na madoa madogo. Mayai hutumiwa na mbuni jike wakati wa mchana na kutamiwa na mbuni dume wakati wa usiku . Mayai huanguliwa baada ya siku 35-45, na kisha hapo mbuni jike na dume wote hushirikiana kuwakuza watoto wao. Mbuni weusi huwindwa wakati huu, na mara nyingi mbuni mtoto mmoja tu ndiyo hufanikiwa kukua, huku wengine wakigeuzwa kitoweo na wanyama wengine wala nyama. Mbuni wanaokuzwa na binadamu, huhamisha sana upendo wao, na kuanza kuwapenda sana binadamu wanaowatunza.

Shamba la Mbuni la Ketola huko Nurmijärvi, Ufini.[1][2]

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia[hariri | hariri chanzo]

  • Struthio anderssoni - spishi kutoka mayai(?)
  • Struthio asiaticus (Asian Ostrich) (Asia ya kati mpaka China, mwanzo wa Pliocene - mwisho wa Pleistocene)
  • Struthio brachydactylus (Ukraine, Pliocene)
  • Struthio chersonensis (Ulaya wa kusini mashariki mpaka Asia ya magharibi ya kati, Pliocene) - spishi kutoka mayai
  • Struthio coppensi (Elizabethfeld, Namibia, mwanzo wa Miocene)
  • Struthio daberasensis (Namibia, mwanzo - kati ya Pliocene) - spishi kutoka mayai
  • Struthio dmanisensis (Dmanisi, Georgia, mwisho wa Pliocene/mwanzo wa Pleistocene)
  • Struthio kakesiensis (Laetoli, Tanzania, mwanzo wa Pliocene) - spishi kutoka mayai
  • Struthio karingarabensis (Afrika ya kusini magharibi na kati, mwisho wa Miocene - mwanzo wa Pliocene) - spishi kutoka mayai(?)
  • Struthio linxiaensis (Yangwapuzijifang, China, mwisho wa Miocene)
  • Struthio oldawayi (Tanzania, mwanzo wa Pleistocene - labda spishi ndogo ya S. camelus)
  • Struthio orlovi (Moldova, mwisho wa Miocene)
  • Struthio wimani (China na Mongolia, mwanzo wa Pliocene)

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]