Majadiliano:Mbuni

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbuni ni ndege wakubwa wa familia Struthionidae. Kuna spishi mbili katika jenasi moja, lakini wataalamu wengine wanafikiri ni spishi moja tu. Ndege hawa ni wakubwa kuliko wengine wote. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na wanaweza kukimbia sana, hata kwa mwendo wa km 65 kwa saa, lakini hawawezi kuruka angani. Rangi za manyoya ya dume ni nyeusi na nyeupe na rangi ya ngozi yake (shingo na miguu) ni nyekundu, pinki au buluu kufuata na nususpishi. Manyoya ya jike ni kahawiakijivu na rangi ya ngozi ni sawa na dume. Mbuni wanaishi savana, nyika na majangwa ya Afrika, lakini wanafugwa ulimwengu wote. Jina la sayansi la spishi kuu, Struthio camelus, linatoka lugha ya Kiyunani: στρουθιον = jurawa na καμηλος = ngamia.

Dume la mbuni ana harimi ya majike 2-7 lakini moja tu anatawala. Dume hupanda majike yote ya harimi yake na majike huyataga mayai yao yote katika tago moja ambalo dume amelitengeneza. Jike anayetawala hutaga kwanza na baadaye hutupa mayai ya majike wasio na nguvu sana. Kwa kawaida hubakisha mnamo mayai 20. Majike huyaatamia mayai mchana na dume huifanya usiku, kwa sababu rangi ya jike inafanana na mchanga na rangi ya nyeusi ya dume haionekani usiku.

Laurent salaam. Umeweka hapa nakala ya aya mbili za makala ya mbuni, lakini sifahamu sababu. Unaweza kueleza tafadhali? Asante. ChriKo (majadiliano) 15:23, 19 Mei 2019 (UTC)[jibu]

Msambao au uenezi?[hariri chanzo]

Riccardo salaam. Niliona kuwa umebadilisha msambazo kwa uenezi. Nakubali kwamba wakati nilichagua msambazo, nilifanya makosa. Inapaswa kuwa msambao. Sina hakika kuwa uenezi ni bora. Labda maneno hayo mawili ni visawe, lakini nadhani msambao unaelezea vizuri zaidi "distribution of a species". Amani kwako. ChriKo (majadiliano) 14:34, 29 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Ndugu, nafurahi kupata ujumbe kutoka kwako. Sijawahi kusikia neno "msambao" na katika KKK halimo, ila si baya, linaeleweka. Katika KKK "uenezi" ni kisawe cha "ueneaji", kwa hiyo ni sahihi. Lakini ukipenda kubadilisha, kwangu ni sawa, usiogope!!! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:47, 29 Juni 2021 (UTC)[jibu]
Asante ndugu. Unaweza kuona "msambao" katika Kamusi Awali ya Sayansi na Teknolojia. Siku njema. ChriKo (majadiliano) 07:45, 30 Juni 2021 (UTC)[jibu]