Ziwa Manyara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

3°35′S 35°50′E / 3.583°S 35.833°E / -3.583; 35.833

Ziwa Manyara

Ziwa Manyara ni moja kati ya maziwa ya Tanzania. Linapatikana kaskazini mashariki, katika Mkoa wa Manyara, Wilaya ya Babati.

Lipo ndani ya Bonde la Ufa na ndani ya hifadhi ya taifa likiwa kivutio kikubwa kwa watalii kutokana na wingi wa ndege aina ya korongo walio na mvuto mkubwa kwa kila mtu. Ndege hao huonekana kama pazia kubwa jeupe nyakati za mchana wanapokuwa ziwani kujipatia chakula na mapumziko.

Ukubwa wake ni km2 231. Kina chake hakizidi mita 3.7.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]