Ziwa Kitangiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Samaki huyu anaaminika kuvuliwa katika ziwa Kitangiri; picha yake inapatikana katika makumbusho ya London.

Ziwa Kitangiri ni kati ya maziwa madogo ya Tanzania.

Linapatikana katika mkoa wa Singida, wilaya ya Iramba, tarafa za Shelui na Kisiriri. Shughuli zifanywazo katika ziwa hili ni uvuvi wa samaki wa aina mbalimbali kama vile: kambale, kamongo, perege, nembe na ningu. Ziwa Kitangiri limekuwa chanzo kikubwa cha uchumi katika wilaya ya Iramba.

Kuna wanyama wengine waishio humo kama vile kiboko n.k.

Pia kuna ndege wengi wa aina mbalimbali wazuri wa kuvutia; ndege hao ni: flamingo, korongo, ndegemwambu (bwana usafi), fongafonga, batamaji, batamzinga n.k.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]