Nenda kwa yaliyomo

Ikuza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ikuza ni jina la kisiwa katika Ziwa Viktoria, la pili duniani kwa ukubwa, pia la kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35540 [1].

Kata inaundwa na vijiji vya Ikuza na Kasenyi.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,870 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,978 waishio humo.[3]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kwa asili wakazi wa kisiwa hiki ni Wahaya na Wazinza, ambao wamehamia huko wakitokea kisiwa cha Rubondo na wengine wakitokea ng`ambo ya Kimwani.

Miaka ya 1970 hadi 2000, Ikuza ilikuwa kisiwa chenye kijiji kimoja tu ambacho kilikuwa na vitongoji vya Msenyi-Lwazi, Nyamahanzu, Kazilantemwa-Ibanga na Mlwoga. Kisiwa kilihudumiwa na shule moja iliyoitwa Shule ya Msingi Ikuza.

Kutokana na mahitaji ya wananchi wa kisiwa hicho, serikali iligawa vitongoji kuwa vijiji kama ilivyo hadi leo ambapo kisiwa hicho kina hadhi ya kata. sawa na Kataya kisiwa cha Mazinga, kata ya Kimwani, kata ya Bumbile na kata nyingine zinazounda wilaya ya Muleba katika mkoa wa Kagera.

Wakazi wa kisiwa hiki walijishughulisha na kilimo cha mazao ya migomba na mihogo pamoja na mibuni.

Kisha miaka ya 2000 wakagundua uvuvi wa samaki na dagaa ambao umeweza kupandisha unafuu wa maisha ya wakazi wa kisiwa hiki.

Kutokana na sera nzuri za nchi, Watanzania wengi wamekijua kisiwa hiki na umaarufu wa uvuvi unadhihirika pale unapotembelea makambi ya Kasenyi, Kazilantemwa, Nyarugusu na Lwazi pamoja na eneo la Nyamahanzu. Uvuvi wa dagaa nao ukatangaza kisiwa hiki nje ya mipaka ya nchi, wanunuzi wa bidhaa hiyo kutoka Rwanda, Congo-Zaire na nchi zinazozunguka ziwa Victoria wakaingia kupata bidhaa hiyo. Si miaka mingi kisiwa hiki kimeinuka kiuchumi na kinazidi kukua.

Usafiri kuingia na kutoka kisiwa hiki ni maboti ya mbao ambayo yanahudumia kila kona ya kisiwa hiki kwa utaratibu na ustaarabu, mabaharia wakitumia ujuzi na ukarimu kuvutia biashara yao isipungue wateja kama vilivyo visiwa vingine ambapo hutumia maboti kufika maeneo mbalimbali, kwa kuwa kisiwa cha Ikuza kinategemea sana wasafiri wanaotokea nchi kavu, kama vile Muleba na Chato, kupitia Magarini. Kuna vituo mbalimbali vya kuingilia, kama vile Chakazimbwe, Rwazi, Nyarugusu, pamoja na Kasenyi, ingawa inaonekana kuwa vituo vikuu ni Katunguru kwenda Ikuza, Mganza mpaka Ikuza, Kimwani Magarini kuingia na kutoka.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 172
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ikuza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.