Biirabo
Biirabo ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35521 [1].
Kuna vijiji kama Kanywangonge, Katobago, Bugarama, Kihumulo, Biirabo na Kabare. Kijiji cha Kanywangonge kina vitongoji vitano: Kanywangonge, Nyamiramba, Kibera, Kamushenge na Rwakaziba.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 18,793 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,900 waishio humo.[3]
Wakazi wanajishughulisha na kilimo hasa cha kahawa kama zao kuu. Katika kijiji cha Kanywangonge shuguli kubwa ni kilimo cha mazao ya mboga.
Kuna shule za msingi saba kama Kanywangonge, Katobago, Bugarama, Kihumulo, Biirabo pamoja na Kabare A na B.
Shule za sekondari ni pamoja na Kihumulo na Biirabo.
Vituo vya afya ni Kabare A na B pamoja na Kanywangonge.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 172
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania |
||
---|---|---|
Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Biirabo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |