Nenda kwa yaliyomo

Kamachumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kamachumu ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35510.[1]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 17,129 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,567 waishio humo.[3]

Kamachumu ni chimbuko mojawapo ya harakati za TAA na TANU chini ya uongozi wa Ali Migeyo (1900 - 1982) ambaye anakumbukwa kwa tukio la kupigwa mabomu ya machozi na kumng'ata Mzungu ambaye katika malalamiko yake alimwita Migeyo kwa jina la Ali Matata. Migeyo alikuwa akihutubia wananchi wa Kamachumu kabla ya zahama ya wakoloni. Mwaka 1953 alifungwa jela na mwaka 1954 alishindwa kuhudhuria mkutano wa kuasisi TANU kutokana na kifungo alichokitumikia hadi mwaka 1961. Baada ya Uhuru alikamatwa na Serikali ya Nyerere na kutupwa gereza la Ukonga hadi mwaka 1965. Haya yameelezwa kwenye kitabu Cha Profesa Gelase R. Mutahaba kinachoitwa Portrait of a Nationalist: The life of Ali Migeyo.

Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kamachumu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.