Buhangaza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Buhangaza ni jina la kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35538 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,603 waishio humo.[2]

Kata hii inaundwa na vijiji vinne ambavyo ni pamoja na Buyaga, Buhangaza, Kashenge na Rwenshato.

Kata hii ina jumla ya shule tatu za msingi ambazo ni pamoja na Buhangaza, Rwenshato na Buyaga, pia ina shule moja ya sekondari ya Ikondo.

Katika kata hii shughuli kuu za kiuchumi ni pamoja na kilimo cha zao la kahawa pamoja na migomba. Shughuli nyingine ndogondogo zinazofanyika katika kata hii pamoja na kilimo, ni biashara, uvuvi na ufugaji.

Chakula cha asili, kama ilivyo kwa mkoa wote wa Kagera, ni ndizi.

Kata hii kijiografia imezungukwa na mto maarufu kwa jina la mto Ngono na milima ya mikunjo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga Kisiwa | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Buhangaza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.