Kisiwa cha Rubondo
Kisiwa cha Rubondo ni kisiwa kimojawapo cha mkoa wa Geita, kaskazini mwa Tanzania, ambacho kinapatikana katika Ziwa Viktoria, ambalo ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani, likiwa linazungukwa na nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda.
Ndipo ilipo hifadhi ya kisiwa cha Rubondo iliyoanzishwa huko kwa sababu kisiwa cha Rubondo ni makazi na mazingira muafaka ya kuzaliana samaki wakiwemo sato na sangara. Sangara huweza kuwa na ukubwa wa hadi kilo 100.
Fukwe za kisiwa hiki ni miongoni mwa makazi ya pongo na nzohe. Aidha hifadhi hii ni maskani makuu ya ndege na samaki kama zumbuli, chechele na taisamaki.
Mbali na ndege hao kisiwa hiki ni makazi ya aina nyingine nyingi za ndege wa majini na mimea kadhaa ambayo hutoa harufu nzuri ya kuvutia.
Wanyama wakazi wa hifadhi hii ni kama viboko, pongo, nzohe, fisi maji, mamba na pimbi ambao wanashirikiana makazi na wanyama waliohamishiwa katika hifadhi hii kama sokwe, tembo, mbega weusi na weupe na twiga.
Namna ya kufika
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 457 na iko kaskazini magharibi mwa Tanzania, katika mkoa wa Geita. Pia hifadhi hii -Inafikika kwa ndege za kukodi kutoka Arusha, Ziwa Manyara, Serengeti na Mwanza. -Kwa njia ya barabara kutoka Mwanza-Sengerema-Geita-Nkome kisha kwa boti hadi hifadhini. -Kwa meli ndogo kutoka Muleba na Bukoba vilevile kwa njia ya barabara kutoka wilaya za Biharamulo na Muleba kupitia kijiji cha Mganza.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Geonames.org
- TANAPA
- Utalii wa Tanzania Archived 13 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- Safiri Tanzania
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |