Nenda kwa yaliyomo

Ziwa Dweru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ziwa George (Uganda))
Mito na maziwa ya Uganda. Bonyeza ili kukuza picha.

Ziwa Dweru (au ziwa George la Uganda) ni ziwa dogo (km2 250) la eneo la Maziwa Makuu ya Afrika.

Liko nchini Uganda kwenye Ikweta.

Ziwa Dweru linachangiwa na mto Nyamwamba na humwaga maji yake kaskazini mwa Ziwa Edward kupitia Mtaro wa Kazinga. Halafu ziwa Edward humwaga maji yake kaskazini kupitia mto Semliki katika ziwa Mwitanzige.

Ndani yake vinapatikana visiwa vya Akika, Irangara, Kankuranga, Kitako na Sikanki.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]