Ziwa Magadi (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ziwa Magadi)
Jump to navigation Jump to search
Lake Magadi
Mahali Bonde la Ufa
Nchi za beseni Kenya
Eneo la maji 100 km²

Ziwa Magadi lipo kusini mwa Kenya katika mkoa wa Bonde la Ufa, kaskazini mashariki mwa Ziwa Eyasi. Wakati wa kiangazi 80% ya ziwa hili huwa limejaa Sodium kabonati na ni maarufu kwa aina mbali mbali za ndege zinazoishi kando kando ya ziwa hilo kwa mfano flamingo.

Ziwa Magadi lina ukubwa wa kilomita 100 mraba na huwa limejaa maji iliyokolea sodium karbonati ambayo huwa na kiasi kikubwa cha madini ya trona. Asili ya chumvi hii ni chemichemi ya moto inayopatikana katika bonde la ufa. Chemichemi hizi huwa kaskazini magharibi na kusini mwa ziwa hili. Wakati wa msimu wa mvua chumvi huwa inapungua ziwani na kisha uzidi tena maji yanapokauka na kuacha chumvi nyeupe. Kuna aina moja tu ya samaki kwenye ziwa hili, cichlid Alcolapia grahami. Samaki huyu anaishi kwenye chemichemi moto zilizo kwenye ufukwe wa ziwa hili.

Ziwa Magadi asili yake haikuwa na kiwango kubwa cha chumvi. Miaka elfu kadhaa iliyopita (kipindi cha Pleistocene) na katikati ya kipindi cha Holocene Ziwa magadi lilikuwa na samaki wengi na kiwango cha chumvi kilikuwa chini. Kuna mda wa kihistoria ambamo Ziwa Magadi na Ziwa Natron zilikuwa zimeshikana kuwa ziwa moja kubwa.

Ziwa Magadi, kutoka anga za mbali .

Mji wa Magadi upo kwenye pwani ya nyanda ya mashariki ya ziwa hili. Kiwanda ca Magadi soda kinapatikana kwenye mji huu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Baker, B.H. 1958. Geology of the Magadi area. Report of the Geological Survey of Kenya, 42, 81 pp.
  • Behr, H.J. 2002. Magadiite and Magadi chert: a critical analysis of the silica sediments in the Lake Magadi Basin, Kenya. SEPM Special Publication 73, p. 257-273.
  • Eugster, H.P. 1970. Chemistry and origin of the brines from Lake Magadi, Kenya. Mineralogical Society of America Special Paper, No. 3, p. 215-235.
  • Eugster, H.P. 1980. Lake Magadi, Kenya, and its Pleistocene precursors. In Nissenbaum, A. (Editor) Hypersaline brines and evaporitic environments. Elsevier, Amsterdam, pp. 195–232.
  • Jones, B.F., Eugster, H.P., and Rettig, S.L. 1977. Hydrochemistry of the Lake Magadi basin, Kenya. Geochimica et Cosmochimica Acta, v. 41, p. 53-72.