Viktoria wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Malkia Victoria)
Malkia Viktoria mwaka 1887.

Malkia Viktoria wa Uingereza (24 Mei 181922 Januari 1901) alikuwa malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania na Ueire tangu 1837 hadi 1901. Hakukuwa na mfalme au malkia mwingine aliyeshika nafasi ya mkuu wa dola kwa muda mrefu zaidi hadi alipopitwa na Elizabeti II.

Alipewa hadhi ya malkia akiwa na umri wa miaka 18. William IV aliyekuwa mfalme alipofariki Viktoria amekuwa mrithi kwa sababu baba yake alikuwa ameshaaga dunia.

Alipokuwa malkia Uingereza ilikuwa tayari ufalme wa kikatiba na madaraka ya mfalme au malkia yameshapungua. Lakini aliheshimiwa sana akawa ishara ya maendeleo na enzi ya Uingereza. Wakati wake nchi iliendelea kuwa yenye nguvu duniani na kujenga utawala juu ya makoloni mengi. Mapinduzi ya viwanda yalifikia kilele chake na Uingereza ilishinda nchi zote za dunia kiteknolojia, kiuchumi na kijeshi.

Kwenye mwisho wa utawala wake uwezo huu umeshapungua kutokana na maendeleo ya nchi kama Ujerumani na Marekani lakini alisimamia milki iliyounganisha theluthi moja ya watu wote duniani sehemu ya tano (20%) ya uso wa dunia.

Kipindi chake huitwa mara nyingi "enzi ya Viktoria".

Mwaka 1840 aliolewa na Albert wa Saksonia-Coburg na Gotha akazaliana naye watoto 9. Albert aliaga dunia mapema mwaka 1861 akiwa na miaka 42 pekee na Viktoria aliendelea kuonyesha huzuni yake kwa kuvaa nguo za mjane kwa miaka mingi iliyofuata.

Wakati Uingereza ilipopanua utawala wake duniani alipewa pia cheo cha kaisari cha Uhindi. Binti yake wa kwanza aliolewa na Kaisari Wilhelm II wa Ujerumani.

Kipindi chake kilikuwa kipindi cha maendeleo ya kiuchumi na matabaka ya juu na ya kati yaliona maendeleo makubwa maishani lakini matabaka ya chini bado yalikuwa na maisha magumu. Hata kama jeshi la Uingereza ilipigana vita vingi duniani katika makoloni yake watu wa Uingereza yenyewe waliona kipindi kirefu cha amani na maendeleo.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Viktoria wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.