Safu ya Ruwenzori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Safu ya Rwenzori kusini ya Fort Portal (Uganda)
Mimea ya pekee ya Rwenzori

Safu ya Ruwenzori (pia: Rwenzori) ni eneo la milima katika Afrika ya Kati kwenye mpaka wa Uganda na JK Kongo. Mlima wa juu ni Pic Marguerite (Mlima Stanley) wenye kimo cha mita 5,109 juu ya UB. Mingine ni mlima Speke (m 4,890), mlima Baker (m 4,844), mlima Emin (m 4,798), mlima Gessi (m 4,715) na mlima Luigi di Savoia (m 4,627).

Baada ya Kilimanjaro na mlima Kenya, Ruwenzori ni mlima mkubwa wa tatu Afrika. Pamoja na hii miwili ndiyo milima pekee yenye barafuto za kudumu kwenye bara la Afrika.

Huaminiwa ya kwamba Rwenzori ni sawa na "Milima ya Mwezi" inayotajwa katika taarifa za Ptolemaio zamani za Misri ya Kale.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Safu ya Ruwenzori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.