Nenda kwa yaliyomo

Kikuyu (lugha)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gikuyu, Kikikuyu
Gĩkũyũ
Inazungumzwa nchini Kenya
Jumla ya wazungumzaji takriban 5,500,000 (1994 I. Larsen BTL)[1].
Familia ya lugha Lugha za Niger-Kongo
Misimbo ya lugha
ISO 639-1 ki
ISO 639-2 kik
ISO 639-3 kik

Kikikuyu (jina la wenyewe: Gĩkũyũ) ni lugha ya Kibantu inayojadiliwa na Wagikuyu ambao watu milioni 5.5 nchini Kenya ni lugha yenye wasemaji wengi katika nchi hii. Kama lugha ya Kibantu ni sehemu ya lugha za Niger-Kongo.

Wasemaji wanaishi kiasili kwenye nyanda za juu za Kenya ya Kati kati ya Nyeri na Nairobi. Siku hizi wanapatikana kote Kenya. Lugha ina vikundi vinne vya lahaja ambazo ni za Kirinyaga, Murang'a, Nyeri na Kiambu.

Gikuyu inafanana kwa kiasi kikubwa na Kiembu, Kimeru na Kikamba.

Fasihi na media

[hariri | hariri chanzo]

Tangu zamani za koloni Gikuyu imewahi kuandikwa. Vitabu vya kwanza kwa Gikuyu vilikuwa Biblia na vitabu vya ibada. Tangu uhuru waandishi mbalimbali walianza kuandika. Anayejulikana zaidi ni Ngugi wa Thiong'o na kati ya riwaya zake iko "Mũrogi wa Kagogo". Waandishi wengine ni Mwangi wa Mutahi na Gatua wa Mbugwa.

Mjini Nairobi kuna pia rungoya ya Gikuyu na pia vipindi vya tyubu.

  1. http://www.ethnologue.com/language/kik Accessed 2007/07/09

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikipedia
Wikipedia
Kikuyu (lugha) ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru