Nenda kwa yaliyomo

Milima ya Ngong

Majiranukta: 1°24′S 36°38′E / 1.400°S 36.633°E / -1.400; 36.633
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vilima vya ngong)
Milima ya Ngong.

Milima ya Ngong ni vilele katika safu ya milima na vilima inayopatikana katika kaunti ya Kajiado, kusini mwa Kenya, upande wa mashariki ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Iko kusini magharibi karibu na Nairobi.

"Ngong" ni neno la Kimaasai maana "nguyu"[1] kutokana na vilele 4 vya mabonde, ambavyo vimesimama peke yake kupanda kutoka tambarare kuzunguka Nairobi.

Vilima vya Ngong, kutoka mteremko wa mashariki, vinaangalia Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, na kaskazini mwa mji wa Nairobi. Vilima vya Ngong, kutoka mteremko wa magharibi, vinaangalia Bonde la Ufa futi 4000 chini, ambapo vijiji vya Wamaasai vimekua vikiendelezwa.

Kimo cha milima ya Ngong ni mita 1961 katika urefu, lakini urefu wa milima ni kama mita 2460 juu ya usawa wa bahari[2][3] Katika miaka ya utawala wa ukoloni wa Uingereza, eneo kuzunguka vilima vya Ngong ilikuwa sehemu ya kilimo ya walowezi, nyumba nyingi za jadi za ukoloni bado zinaonekana katika eneo hilo.

Ngong divisheni ina vitongoji vya Nairobi kama Ongata Rongai, Kiserian, Matasia na Kitengela ambapo wakazi (ambao kimsingi ni wa Nairobi) hujenga nyumba katika maeneo ya utulivu mkubwa kuliko ya mji.

Katika filamu ya 1985 Out of Africa, vilele vinne vya Ngong hutokea katika usuli kadhaa karibu na nyumba ya Karen Blixen's. Bado wakazi wa mitaa huripoti kuona simba katika vilima wakati wa miaka ya 1990.

Kaburi la wapweke la Denys Finch Hatton, iliyo na alama ya obelisk na bustani, iko kwenye mteremko wa mashariki wa vilima vya Ngong, inayoelekea hifadhi kubwa ya mbuga. Milima ya Ngong, kutoka mteremko wa mashariki, inatazama Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi na mbali zaidi jiji la Nairobi. Milima ya Ngong upanda wa magharibi inatelemka moja kwa moja hadi bonde la ufa zaidi ya mita 1200 chini.

Karibu na milima iko mji wa Ngong. Mwinuko wa mji wa Ngong kwenye mguu wa milima ni mita 2061 ju ya UB.[4]

Shamba la upepo linajengwa milimani.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "FOUR DAYS - OLOGASAILE / MAGADI(BEAS 08)" (tour), Government of Kenya, 2006, BreakawayExpedition.com webpage: BreakawayExpedition-Tour.
  2. Aeronautical chart for Nairobi area 1:1,000,000 scale
  3. "Ngong, Kenya Page" (statistics), Falling Rain Genomics, Inc., 2004, FallingRain.com webpage: FallingRainCom-Ngong.
  4. "Ngong, Kenya Page" (statistics), Falling Rain Genomics, Inc., 2004, FallingRain.com webpage:FallingRainCom-Ngong.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

1°24′S 36°38′E / 1.400°S 36.633°E / -1.400; 36.633